September 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Vodacom na chama cha gofu waungana kuunga mkono mchezo huo

VODACOM Tanzania Plc kwa kushirikiana na Chama cha Gofu Tanzania, imejitokeza kama mdhamini mkuu wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open, yanayotarajia ushiriki wa wachezaji zaidi ya 150 wa gofu kutoka Tanzania na nchi za mashariki na kusini mwa Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuendeleza michezo ya gofu katika msimu wa tatu hapa jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar. Vodacom ikiwa inaadhimisha miaka 25 inalenga kujikita kama mtandao namba moja unaounga mkono mchezo wa gofu nchini Tanzania.

Tanzania Open si mashindano pekee, bali ni jukwaa la kuonesha vipaji, mshikamano katika michezo na ubunifu wa kidijitali. Kupitia ubia huu, Vodacom inaleta mapinduzi katika mchezo wa gofu kwa kuunganisha urithi wa mchezo huu na teknolojia ya kisasa, huku ikikuza ushirikishwaji wa jamii na ujumuishi kwenye michezo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano haya, Mkuu wa idara ya masoko na uwezeshaji Vodacom Business, Joseph Sayi, alisema:

Ushirikiano wetu na Tanzania Open unaonyesha dhamira ya Vodacom katika kukuza michezo nchini Tanzania huku tukionesha namna teknolojia inavyoweza kuboresha maisha ya wananchi hata kupitia michezo. Kuanzia huduma za mtandao hadi huduma za malipo kwa kutumia M-Pesa, tunahakikisha kila mmoja anapata uzoefu wa kipekee ndani na nje ya uwanja.”

Pia, mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania, Gilman Kasiga, alisema: Mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2025 ni tukio la kihistoria kwa mchezo wa gofu na kwa taifa letu. Kwa mwaka wa tatu mfululizo, Vodacom imeendelea kuwa bega kwa bega nasi kama mdhamini mkuu, jambo linalodhihirisha dhamira yao ya kuendeleza michezo na kukuza vipaji nchini. Kama mashindano makuu ya Chama cha Gofu Tanzania, Vodacom Tanzania Open siyo tu jukwaa la kuonesha umahiri wa wachezaji wetu wa kulipwa na wale wa kiwango cha juu, bali pia ni chanzo cha hamasa na matumaini kwa kizazi kipya cha wachezaji.

Tunajivunia kuona vijana, wanawake, na wachezaji chipukizi wakishiriki kwa pamoja, jambo linaloashiria dhamira ya dhati ya TGU katika kukuza ushirikishwaji, maendeleo, na ukuaji endelevu wa mchezo huu. Kupitia ushirikiano wetu naVodacom, tunaonesha namna ambavyo gofu si mchezo pekee bali ni nyenzo ya kukuza utalii, uwekezaji, ajira na fursa nyingi za kijamii na kiuchumi nchini Tanzania. Mashindano haya ni ya ubora wa kimataifa, na tunawaalika wadau wote wa gofu pamoja na umma kushiriki nasi katika kusherehekea mchezo huu wa heshima na hadhi ya kipekee

Kwa kuhitimisha, Mkuu wa idara ya masoko na uwezeshajiVodacom Business, Joseph Sayi, alieleza:

Vodacom Tanzania Open ni mfano halisi wa kuunganisha urithi wa michezo na ubunifu wa teknolojia ya kisasa. Sisi Vodacom tunajivunia kuwa sehemu ya mashindano haya.

Ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Chama cha Gofu Tanzania ni hatua kubwa katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya gofu ya kikanda, huku ikisukuma mbele dhamira ya Vodacom ya jamii iliyounganishwa kidijitali.

About The Author

error: Content is protected !!