
TUNDU Lissu – Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), adai kuwa mchakato wa mkuhamisha kesi ya uhaini inayomkabili kutoka kwenye mahakama ya Haki Mkazi Kisutu ni batili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kesi hiyo Na. 19605/2025 inayosikilizwa na jopo la majaji watatu Jaji Dunstan Nduguru, Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde ikiwa katika hatua za usikilizwaji wa awali (PH) , Lissu ameomba mahakama Kuu kutolitambua shauri hilo kwa kuwa halina miguu ya kisheria kwa kulikuwa na makosa ya msingi katika taratibu za ukabidhi wa kesi (committal proceedings) yaliyofanyika Kisutu, hali inayoharibu mchakato mzima.
Jana tarehe 8 Septemba 2025, Jopo la majaji lilisikiliza hoja hizo na kuagiza nyaraka husika zisomwe rasmi mahakamani. Ilibainika kuwa kulikuwa na makosa kadhaa katika nyaraka hizo, jambo lililolazimu Lissu.
Katika hatua nyingine, Lissu aliomba apewe muda zaidi kusoma nyaraka za mwenendo wa kesi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai nyaraka alizopewa akiwa gerezani hazikuwa kamili. Mahakama ilikubali, ikampa muda wa saa moja kuzisoma tena.
Baadaye, Lissu alirejea mahakamani na kueleza kuwa bado kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya nyaraka alizopewa na zile alizopelekewa akiwa gerezani na akaomba apewe usiku mmoja zaidi kuzisoma kwa kina. Mahakama ilikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi leo.
Awali, upande wa mashtaka ulieleza kuwa kesi hiyo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya kusomewa hoja za awali, lakini utekelezaji wake ulikwama kutokana na notisi iliyoletwa na mshtakiwa kupitia Mkuu wa Gereza la Ukonga, akiomba kuwasilisha pingamizi la kupinga mamlaka ya mahakama na uhalali wa hati ya mashtaka.
Leo Lissu tarehe 9 Septemba Lissu anaendelea na utetezi wa hoja yake….(endelea):-
Mh. Jaji nashukuru, jana nilipewa nafasi nikasome. Sasa hiyo kazi nimeifanya usiku kucha kwahiyo naomba kwa kuanzia nieleze tofauti zilizopo kati ya hizi nyaraka mbili na ili nisiwachanganye ninaposema rekodi ya Ukonga maana yake ni ile niliyoletewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu na Hakimu Franco Kiswaga, ndio alimpa Kamishina msaidizi wa Polisi Rabi Stima.
Rekodi ya Ukonga nina maana ni hiyo nyaraka niliyoletewa na Hakimu Kiswaga. Kwahiyo nikisema rekodi ya Mahakama hii nitakuwa namaanisha ile niliyopewa jana.
Sasa naomba nianze.
1. Utofauti wa rekodi ya Ukonga ina kurasa 16 tu. Rekodi ya Mahakama hii ina kurasa 101. Sasa hizo kurasa zingine zilikuwa wapi? Nyaraka za mahakama zinawezaje kuwa na utofauti wa namna hii? Katuga hawakumpa hii niliyonayo mimi. 2. Rekodi ya Ukonga haina ile scanned berg (kibox pembeni kulia) inamaanisha ni original. Sasa ya ukonga haina lakini niliyopewa jana inazo hizo scanned berg. Sasa ililetwa na mahakama lakini sio original.
3. Rekodi ya ukonga inaanza tarehe 18/08 na inaishia Tar. 18/08. Kwa kifupi ilianza siku hiyo hiyo na kuishia siku hiyohiyo. Kesi ilianza na kumalizika siku hiyohiyo. Rekodi ya Mahakama hii imeanzia April 10, 2025 na kuishia Agosti 18, 2025. Mliyonipa hapa ilikuwa imekamilika kwa kila kitu.
4. Ukurasa wa 1 wa rekodi ya Ukonga na Ukurasa wa 86 wa rekodi ya Mahakama hii. Ukiangalia ile ya Ukonga page 1 ni kwamba commitall proceedings ilianza immediately. Yani mwanzo pale committal proceedings, open evident on itself lakini kwenye rekodi ya mahakama hii ukurasa wa 86 kulikuwa na ubishani mkubwa sana ambao umerekodiwa. Utaona baada ya corum kuna heading inaitwa Proveedings Mr. Katuga alielezea mambo kadhaaa…. ilianza hivyo. Kinachofuata kuanzia page 86 hadi 89 ni submissions kati ya prosecution na mimi mwenyewe. Rekodi ya ukonga mabishano hayo hayapo kabisa. Lakini hii niliyopewa hapa kila kitu kipo.
Utaona kwa mfano ukurasa wa 87 rekodi ya mahakama hii Hakimu alisema nimezingatia mawasilisho ya pande zote. Na akatambua uamuzi wa mahakama kuu. Mambo hayo kwenye document nikiyoletewa hayakuwepo na hakuambatanisha.
6. Kwenye ukurasa wa 15 wa rekodi ya Ukonga kuna orodha ya mashahidi halafu kuna maneno kuwa na mimi mshitakiwa I will Call the Following Witnesses
Lakini kwenye ukurasa wa 100 wa rekodi ya Mahakama hii inasema I will call my witnesses and I will have my Advocates.
Kwenye rekodi ya ukonga na kwenye orodha ya mahakama hii hawajaandikwa mashahidi wangu. Sio kwamba hawakuwepo, niliwataja lakini nyaraka hizi hazina majina hayo.
1. Samia Suluhu Hassan
2. Isdory Mpango
3. Kassim Majaliwa
Hao wote niliwataja lakini hawakuandika kabisa.
Nitarudi kwenye hilo la majina baadae.
Lakini ieleweke kuwa majina hayo nilitaja mchana kweupe kila mtu alisikia na ilikuwa kwenye Open Court. Aliamua kwa matakwa yake mwenyewe kutokuyaandika.
Hizi nyaraka zote zimetoka Kisutu na zinadai kuwa ni committal proceedings.
Which one is forgery and which one is original.
Mahakama hii inapaswa kujibu why this differences?
Jana niligusia kidogo kwamba kulikuwa na maahirisho mengi sana.
Nilisema yalikuwa zaidi ya 10 hayo maahirisho. Niliposoma usiku nimegundua iliahirishwa mara 13.
Kesi inapoahirishwa kwenye commitall proceedings s. 265(1) the court must record the reason of adjournment and for reasonable cause that adjournment can be granted.
Na hiyo sababu ya msingi lazima iandikwe katika mwenendo.
Sasa nataka nioneshe namna mahakama ya Mheshimiwa. Franco Kiswaga ilivyoheshimu huo utaratibu wa kisheria.
Waheshimiwa majaji ahirisho la kwanza ni Tar. 10 Aprili 2025.
Page. 2 ya rekodi ya mahakama hii para ya mwisho Mahakama ilisema since this Court has no jurisdiction to hear this matter na hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuahirisha.
Hiyo sio sababu ya msingi kuahirisha kesi. Sasa committal Court haina mamlaka huwezi ahirisha kesi kwasababu hiyo maana mahakama hiyo haina hiyo mamlaka.
Hilo ahirisho hali ku comply na kifungu cha 265(1) cha CPA sababu ilipaswa kuwa labda upelelezi haujakamilika na kwasababu zipi ni wasilisho langu hicho kifungu hakikuzingatiwa kabisa.
Ahirisho la 2 la Tarehe 24 Aprili 2025. Rekodi ya Mahakama hii mtaona kulikuwa na mvutano mkubwa wa kisheria na huo mvutano upo page 5 hadi page 18 ile rekodi nyingi ya Ukonga haya hayapo kabisa.
Kwasababu ya huo mvutano Mh. Hakimu aliandika uamuzi page 13 hadi 18.
Kilichokuwa kinabishaniwa haikuwa uahirishaji tena ikawa ni inshu ambayo kesi isikilizwe vipi?
Mambo ya kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.
Ahirisho lilisema Tar. 06/05 na mtuhumiwa abaki anashikiliwa.
Hapa napo sababu ziko wapi za kuahirisha hii kesi?
Hazikuwepo kabisa sijui alimpelekea nani au aliziandika kwa nani?
Tarehe 06 Mei 2025, na ikaleta mvutano mwingine mkubwa ambao upo page 19 to 20 ya rekodi ya mahakama hii kulikuwa na submissions za kutosha.
Ahirisho lililotolewa na mahakama lilisema hivi sababu za upande wa mashitaka hazina maana.
Anasema page 20 kwamba duty to prosec to expedite the investigation of the case na ninawataka waje waeleze wamefikia wapi Tarehe. 19 Mei
Sasa hii ni sababu ya kuahirisha kesi? I don’t think so.
ZINAZOFANANA
OMO, Mwinyi jino kwa jino urais Zanzibar
Mpina ashinda kesi, mahakama yamruhusu kurudisha fomu
TMA yatangaza utabiri wa mvua za vuli za Oktoba mpaka Desemba