August 31, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Samia: Tuchagueni tunatekeleza kwa uhakika, siyo ‘tone tone’

Rais Samia Suluhu Hassan

 

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema chama hicho kinatekeleza mambo kwa uhakika siyo ‘tone tone’ hivyo amewaomba Watanzania kukichagua katika uchaguzi mkuu wa Oktoba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Samia akiwa jimboni Kondoa mkoani Dodoma, leo tarehe 31 Agosti 2025, amewasihi Watanzania kuchagua mafiga matatu (wabunge, madiwani na Rais wote wa CCM), ifakapo Oktoba 29, siku ya kupiga kura.

“Chagueni mafiga matatu, Serikali haendi na tone tone bali inatoa fedha za maendeleo. Tunapotoa fedha madiwani hawa ndio Bunge lenu, ambapo wanakaa na kuangalia fedha zilizoletwa na miradi iliyopangwa, itekelezwe vipi ili kusimamia,” amesema.

“Najiombea kura mimi, lakini nawaombee madiwani na wabunge ili wakasimamie kazi hiyo. Naomba niletee hawa, watakuja kunadi ilani ya CCM, niwaombe sana Oktoba 29, twende tukakipigie kura CCM,” ameongeza Dk.Samia.

Dk. Samia amesema CCM, ndiyo chama kinachojali utu na mtu, ndio maana kimekuja na kauli mbiu ya ‘Kazi na Utu, Tunasonga Mbele’.

Amewaahidi mambo makubwa wananchi wa Chamwino, Chemba na Kondoa endapo watampa tena ridhaa ya kuongoza Serikali.

About The Author

error: Content is protected !!