
CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemvua uanachama Monalisa Ndallala, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa ya chama hicho. Anatipoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Monalisa amevuliwa unachama huo, kupitia
Tawi lake la Mafifi, kata ya Kihesa mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Monalisa anatuhumiwa kushindwa kutekeleza matakwa ya Katiba ya ACT-Wazalendo, hatua ambayo inatajwa kuhusiana na mvutano wa karibuni juu ya uteuzi wa mgombea urais.
Barua ya ACT- Wazalendo ya tarehe 28 Agosti 2025, iliyosainiwa na Neema Ernest Kivamba, Katibu wa tawi hilo, kwenda kwa Monalisa, imeeleza kuwa kikao cha tathmini cha Kamati ya Uongozi, kilibaini Ndala amepoteza sifa za kuwa mwanachama hai chini ya Katiba ya chama ya mwaka 2015 (toleo la 2024).
“…umepoteza sifa za kuwa Mwanachama halali na hai wa Chama cha ACT Wazalendo kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015 Toleo la Mwaka 2024, Ibara ya 8 (2) (a) (b) na Ibara ya 13 (1) (c) (d) Pamoja na Ibara ya 97 (b) (d)”, imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Uamuzi huo umeambatana na kufutwa kwa kadi yake ya uanachama na kuondolewa jina lake katika regista ya wanachama wa Tawi la Mafifi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Monalisa kupinga uhalali wa mchakato wa uteuzi wa Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, akidai ulikiuka kanuni kwa kuwa Mpina alijiunga na chama tarehe 5 Agosti 2025, nje ya muda rasmi wa kurejesha fomu.
ZINAZOFANANA
Rais Samia kuunda tume ya maridhiano, upatanishi
Kikwete: Wanaopinga uteuzi wa Rais Samia wana roho ya korosho
Mahakama yakubali Chadema kumshitaki Msajili, yazuia kutowatambua viongozi wake