
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amesema kama akichaguliwa kuongoza tena ataunda tume ya maridhiano na upatanishi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Anaripoti Salehe Mohamed, Dar es Salaam … (endelea).
Amesema tume hiyo itasaidia pia kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya hivyo amewaomba Watanzania washirikiane na CCM kwenye safari ya maendeleo.
Ahadi hiyo ameitoa leo, tarehe 28 Agosti 2025 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Kawe alipokuwa akifungua kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba mwaka huu
‘Ndugu zangu wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara na makundi mbalimbali ninawaomba tushirikiane kwa pamoja kuboresha maisha yetu na kuchochea maendeleo ya taifa letu, chama cha kuyafanya hayo mazuri ni CCM nawaombeni mtupe ridhaa ya kuongoza nchi yetu kwa miaka mitano ijayo” amesema Rais Samia
Rais Samia amesema kuwa katika siku 100 za mwanzo iwapo atachaguliwa atahakikisha sheria ya bima ya afya kwa wote inazinduliwa ambapo wataanza na makundi.
“Makundi tutatakayoanza nayo ni wazee, wajawazito, watoto na makundi mbalimbali ambapo gharama zao zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Gharama za matibabu zitabebwa na mfuko huo
Rais Samia amesema pia Serikali itaanza kugharimia matibabu ya kibingwa kwa watu wasijiweza ambayo yamekuwa yakiwafanya watu wshindwe kumudu gharama zake.
“Tutagharimia magonjwa ya saratani, figo, moyo na mifupa ya yale ya fahamu ambayo wananchi wanashindwa kumudu gharama zao. Pia tutaajiri wahudumu wa sekta ya afya 5000” amesema.
Rais Samia amesema katika siku hizo 100, watapiga marufuku tabia ya viongozi wa hospitali na vituo vya afya wa kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zao hadi gharama za matibabu alizozitumia zilipwe.
“Sasa maiti hazitazuiliwa hata kama kuna deni, tutakuja na mfumo wa kuhakikisha jamaa na ndugu wanalipa fedha za hizo wakati wameshamzika mpendwa wao” amesema.
Rais Samia amesema kuwa katika sekta ya elimu watahakikisha kila mtoto wa darasa la tatu anajua kusoma na kuandika na kwa kuanzia wataajiri walimu 7000.
“Tutakuja pia na utaratibu utakaowezesha wanafunzi wa VETA kuchukuliwa na viwanda kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi. Jamani anawaombeni mtuchague CCM tufanye mambo haya ndani ya siku 100” amesema
Rais Samia pia amesema katika siku hizo watatenga Sh. 200 bilioni zitakazotumika kuwasaidia mitaji wajasiriamali na wale wanaoanzisha kampuni changa.
ZINAZOFANANA
Kikwete: Wanaopinga uteuzi wa Rais Samia wana roho ya korosho
Mahakama yakubali Chadema kumshitaki Msajili, yazuia kutowatambua viongozi wake
Pigo jingine ACT- Wazalendo lanukia