
LICHA ya kushindwa kwenye kura za maoni katika majimbo yao Ester Matiko (Tarime Vijijini) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imewateua kuwa wagombea wa ubunge katika majimbo hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Leo tarehe 23 Agosti 2025, Amos Makalla – Katibu wa Uenezi wa Chama hicho ametangaza kuwa Kamati Kuu ya CCM imewateuwa wawili huo kuwa wagombe wa ubunge katika majimbo hayo yaliyopo katika Mkoa wa Mara.
Bulaya na wenzake alitimkia CCM siku chache baada ya bunge kuvunjwa wakiwa bungeni kwa kivuli cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kama wabunge wa viti maalum.
Wengine walioteuliwa na Kama kuu hii ni Jesca Kishoa ameteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iramba huku Hawa Mwaifunga akiteuliwa Tabora Mjini.
ZINAZOFANANA
ACT-Wazalendo wamjibu Polepole
Tutende haki, tutavuna amani
Kesi ya Lissu yapelekwa Mahakama Kuu.