
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbozi imemtia hatiani Athumani Mohamed Mtimbwa (35) mfanyabiashara kwa kosa la kubaka na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kulipa fidia ya Sh. 1 milioni kwa muhanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbozi, Songwe … (endelea).
Mtimbwa alikamatwa tarehe 21 Oktoba 2024, maeneo ya kiwandani Mlowo Wilaya ya Mbozi, ilielezwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo la ubakaji kwa kumvizia muhanga ambaye ni mwanafunzi wa darasa la awali mwenye umri wa miaka minne akiwa anatoka shule na kumvuta kwa nguvu kisha kumuingiza katika kibanda chake cha biashara na kumbaka.
Akitoa hukumu hiyo tarehe 29 Julai 2025, kesi namba 32392 ya mwaka 2024, Hakimu mkazi wa Wilaya ya Mbozi, Nemes Chami alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Mshtakiwa amehukumiwa kifungo pamoja na fidia hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto.
ZINAZOFANANA
Mawakili wa Polepole watoa tamko
Polisi yasisitiza kumtaka Polepole kwa mahojiano
Mahakama yafafanua mashtaka ya Lissu kuhusu hukumu yake