August 7, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Job Ndugai afariki Dunia

Marehemu Job Ndugai

 

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Jijini Dodoma Job Ndugai amefariki Dunia leo tarehe 06 Agosti 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa ya Kifo cha Spika huyo mstaafu imetolewa na Spika wa Sasa wa Bunge Tulia Akson, kupitia taarifa kwa Umma.

“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya Kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo Jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Kongwa, mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika

About The Author

error: Content is protected !!