
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania, kupitia kitengo cha Vodacom Business kinachoshughulika na wafanyabiashara wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa michezo, wamekabidhi tuzo na zawadi kwa washindi tofauti wa mashindano ya golf yaliyofanyika katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hafla hiyo ilikuwa sehemu ya mashindano ya Vodacom Corporate Masters, yaliyolenga kuhamasisha ushiriki wa wadau kutoka sekta mbalimbali kupitia michezo ya kijamii kama golf. Tuzo hizo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wa kike na wa kiume, wanawake, wanaume pamoja na wachezaji wa golf waliobobea kutoka mashirika tofauti.
Kupitia tukio hili, Vodacom iliendeleza dhamira yake ya kuunga mkono michezo, kukuza vipaji na kudumisha uhusiano wa kijamii na wadau wake wa karibu.

ZINAZOFANANA
Masawe ateuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa TPSF
Pakua App yetu na ushinde, pata bonus hadi Sh. 10,000!
Ulaya yazidi kuwaka, leo ni siku ya Mabingwa na wabashiri