
Mwandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imeendelea na zoezi la utambulisho na kukabidhi jezi maalum na vifaa vitakazotumiwa na washiriki wa mbio hizo kwa mdhamini mkuu wa mbio hizo kampuni ya GSM Group ambayo kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages inadhamini huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu huo sita wa mbio hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Zaidi GSM Group kupitia taasisi yake ya GSM Foundation ni wafadhili muhimu katika agenda tatu ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma ambazo ni kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili wa wakunga hadi kufikia wakunga 200 pamoja na kuanzisha mpango mpya wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism) nchini.
Kama ilivyokuwa kwa wadhamini wengine, zoezi la kuwatembelea na kuwakabidhi vifaa hivyo wadhamini hao, leo pia liliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Rayson Foya, alieambatana na baadhi ya maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki hiyo, Godwin Semunyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Tatiana Massimba.
Wakiwa Makao Makuu ya kampuni ya GSM Group jijini Dar es Salaam, maofisa hao wa NBC walipokelewa na wenyeji wao Mkurugenzi wa GSM Group, Gharib Said Mohamed (GSM), Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni hiyo Mhandisi Hersi Said, Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo, Chenedzo Mupukuta pamoja na maofisa wengine waandamizi wa kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Foya pamoja na kuishukuru kampuni ya GSM Group kwa kuwa mdhamini muhimu wa mbio hizo na hivyo kuwa sehemu ya harakati hizo za kijamii ambazo kwa msimu huu zinalenga kukusanya fedha kiasi cha Sh. 700 milioni zitakazosaidia kufanikisha agenda hizo tatu.
“Tupo hapa kukabidhi vifaa hivi kwa uongozi wa GSM Group kama ishara ya kuheshimu na kutambua mchango wao kwenye mafanikio ya mbio hizi. Udhaminiwa wa GSM Group kwenye mbio hizi unahusisha usambazaji wa maji na vinywaji baridi kwa washiriki takribani 12,000 tunaowatarajia kwenye msimu wa sita wa mbio hizi.
“Zaidi GSM Group wameenda hatua nyingine zaidi ambapo kupitia Taasisi yao ya GSM Foundation wameamua kuwa sehemu ya wafadhili muhimu katika agenda zetu hizi tatu ambazo kimsingi zinagusa uhai wa mama zetu na watoto wakati wa kujifungua huku pia mwaka huu tikiangazia zaidi changamoto ya watoto wenye usonji (autism)’’ aliongeza Foya.
Kwa upande wake Mhandisi Hersi, pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa ushirikiano huo na jitihada zake katika kukuza sekta ya michezo nchini pamoja na kuokoa maisha ya wana jamii, alisema alisema ushirikiano huo unathibitisha jitihada na azma ya pamoja baina ya taasisi hizo mbili katika kukuza afya ya mama na ustawi wa jumla wa jamii.
“GSM Group tunafurahi kuwa mshirika mashuhuri wa benki ya NBC katika kufanikisha kusudi hili lenye nia njema kwa jamii tunayoihudumia. GSM Group tunaamini kwa dhati kuwa juhudi za pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazokabili jamii zetu. Kwa kutumia ujuzi na rasilimali mbalimbali, tunaweza kuongeza athari yetu na kupanua wigo wetu.
Hivyo tunawakaribisha washiriki wengi zaidi waje NBC Marathon kwa kuwa pia tumejipanga kuhakikisha tunakidhi mahitaji yao ya maji na vinywaji vingine baridi,’’ alisema.
Akizungumzia maandalizi ya mbio hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon, Tatiana Masimba alisema mwitikio wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi ni mkubwa huku usajili wa mbio hizi ukiendelea kupitia tovuti ya events.nbc.co.tz ambapo washiriki wanatakiwa kuchangia kiasi cha TZS 45,000 kwa usajili wa mtu mmoja mmoja au 42,000 kwa usajili wa kikundi chenye idadi ya watu 30 au zaidi.
ZINAZOFANANA
Pande Marathon haijapata kutokea
Bashiri na Meridianbet mechi za Europa na Conference leo
Rejesha 10% ya hasara yako kwenye Win&Go