July 4, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Karia mgombea pekee nafasi ya Urais TFF

Wallace Karia, Rais wa TFF

 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace John Karia amesalia kama mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais wa TFF kwenye Uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2025 Jijini Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesema wagombea wanne wa nafasi hiyo wamekosa vigezo (Endorsement) kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi hivyo, Wallace Karia amepita kwenye mchujo wa awali baada ya kupata endorsement 46 kati ya 47.

Kwenye nafasi ya Kamati ya Utendaji ya TFF wamepita Wagombea 10 kati ya Wagombea 17 ambao walifika kwenye usaili wa awali.

Kwa sasa Kamati ya Uchaguzi inasubiri kupokea Rufaa za wagombea ambao watakuwa wamekata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi, Rufaa inapaswa ikatwe ndani ya siku 6.

About The Author

error: Content is protected !!