
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Lazaro Twange amesema changamoto ya hitilafu ya umeme iliyojitokeza katika Mfumo wa Gridi ya Taifa ilisababisha kukosekana kwa umeme kwa maeneo mbalimbali nchini tayari imeshatatuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 29 Juni 2025, Mkurugenzi Twange amewaomba radhi Watanzania kwa changamoto iliyojitokeza ambapo amefafanua wataalamu wa Tanesco, wamepambana na mpaka sasa huduma ya umeme imerejea kama kawaida.
‘’Tunawaomba sana radhi wateja wetu kwa hitilafu iliyojitokeza, sisi hatujisikii vizuri na tunajua umuhumu wa nishati ya umeme katika shughuli za kijamii na kiuchumi lakini mpaka majira ya saa 06:30 mchana tayari huduma ya umeme ilirejea katika maeneo yote yaliyoathirika’’ alifafanua Twange.
Hata hivyo, Twange amewahakikishia Watanzania kuwa TANESCO inaendelea na jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika na kupitia changamoto hii Shirika linaendelea kufanya tathmini kuangalia njia mbadala ya kutatua tatizo kwa haraka.
Haya yanajiri baada ya kutokea changamoto ya hitilafu ya umeme katika mfumo wa Gridi ya Taifa iliyosabisha kukosekana kwa umeme katika mikoa yote iliyopata umeme katika mfumo huo kunzia majira ya saa 02:36 asubuhi na kuanza kurejea majira ya saa 04:16 asubuhi.
ZINAZOFANANA
Julai 11 Mahakama kuamua mapingamizi ya Serikali kesi Lissu
SBL yakabidhi mradi wa maji kwa wakazi 14,000 Kwadelo, Kondoa
Meridianbet yaigusa hospitali ya Palestina Sinza