
KLABU ya Yanga imefanikiwa kuifikia rekodi ya Simba ya kutwaa ubingwa mara nne mfululizo, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Yanga ambao waliipoka ubingwa kwa Simba waliochukua mara nne mfululizo kwenye msimu wa 2021/22 na waliendelea kushikilia taji hiyo na leo wameongeza la nne ya kuwafikia watani wao.
Mabao mawili ya Pacome Zouzoua na Clemant Mzize yalitosha kuipa ubingwa baada ya kufikisha pointi 82 wakifuatiwa na Simba waliomaliza nafasi ya pili wakiwa na pointi 78.
Mchezo huo namba 184 ambao awali ulipangwa kuchezwa tarehe 8 Aprili 2025, ukahairishwa mpaka tarehe 15 mwezi huu lakini hakuchezwa na umechezwa leo.
Yanga baada ya mchezo huo walikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.
ZINAZOFANANA
Pande Marathon haijapata kutokea
Bashiri na Meridianbet mechi za Europa na Conference leo
NBC yakabidhi ‘Kits’ za NBC Dodoma Marathon kwa GSM Group