BISHWADIP DEY, Balozi wa India nchini Tanzania, amesema Tanzania iko katika hatua za mwisho kutengeneza magari yanayotumia umeme na gesi nchini kupitia kiwanda cha kampuni ya GF kilichopo kibaha mkoani Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani …( endelea).
Akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa gari ya Mahindra Scorpio uliofanyika jijini Dar es salaam jana tarehe 21 Juni 2025 alisema uwekezaji huo ni matunda ya uhusiano mwema wa Tanzania na India .
“Mahndra imetambulisha gari mpya katika soko la Tanzania na ukanda wa afrika mashariki lakini magari haya kuanzia mwakani yatakuwa yakitengenezwa nchini Tanzania katika kiwanda cha GF Kilichopo Kibaha mkoani Pwani,” alisema Balozi Dey.
Naye mtendaji mkuu wa kampuni ya GF Mehboob Karmali alisema ujio wa Mahndra nchini ni ukombozi kwani leo wametambulisha gari sokoni na baadaye watazindua gari za umeme na gesi zitakazotengenezwa nchini Tanzania kupitia kiwanda GF likichopo Kibaha mkoni Pwani .
“Tutaanza na magari madogo pickup- double cabin maalumu kwa shunguli za kilimo na wajasiliamali wadogo hasa mashambani,” alisema Karmali.
Karmali alizitaka taasisi za umma na serikiali kwa jumla kujenga tabia ya kununu bidhaa kutoka viwanda vya ndani ili kuvilinda viwanda vyetu na kuongeza pato la taifa na kuokoa pesa ambayo ingetumika kuagiza bidha nje ya nchi .
Kampuni ya GF Automobile imezindua gari aina ya Mahindra Scorpio kwaajili ya matumizi katika bara bara za mazingira tofauti hasa vijijini na gesi kukabiliana mazingira sambamba na kuyalinda.
ZINAZOFANANA
Ramadhani ya furaha kwa wote, Meridianbet yawakumbuka wakazi wa Dar es Salaam
Airtel Tanzania yazindua maduka 17 ya Smart Shops Dar, kukuza huduma za kidijitali
Ripoti ya Kerry ya Taste Charts 2026 yaonyesha ladha za tangawizi, ukwaju na mango chilli kinara mabadiliko ya ladha Afrika