June 19, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Maftaha ajiunga ACT pamoja na wanachama 2,567 wa CUF

 

ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CUF na Mbunge wa zamani wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma, amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Nachuma amejiunga na ACT Wazalendo akiwa pamoja na wanachama wengine 2,567 kutoka CUF. Viongozi wa ngazi ya juu wa ACT Wazalendo, akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Bara, Isihaka Mchinjita, waliongoza mapokezi ya wanachama hao wapya.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, naye alihudhuria tukio hilo muhimu ambalo linatazamwa kama mwendelezo wa kuimarika kwa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Hatua ya Nachuma kujiunga na ACT Wazalendo imeibua mjadala mpana kuhusu mwelekeo wa siasa za upinzani nchini, huku wachambuzi wa mambo wakitafsiri uhamaji huo kama ishara ya kupoteza nguvu CUF na kuongezeka kwa mvuto wa ACT Wazalendo katika maeneo ya kusini mwa Tanzania.

About The Author

error: Content is protected !!