
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), imetangaza kufungua dirisha la maombi ya mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 19 Juni 2025, na Bill Kiwia, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo na kusema imetenga Sh. 916.7 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2025 2026.
Fedha hizo zitawanufaisha jumla ya wanafunzi 99,620 wa mwaka wa kwanza katika ngazi ya za diploma, shahada ya kwanza na shahada za uzamili.
Pia amesema wanafunzi 88000 wa shahada ya kwanza watapangiwa mikopo hiyo.
ZINAZOFANANA
Walimu wapya 120 Magu wapewa mafunzo elekezi
Matokeo ya kitado cha sita ufaulu kuongezeka
DAS Kinondoni aipongeza MONTI International kwa kuibua, kulea vipaji vya watoto