
KIWANDA kikubwa na cha kwanza kutengeneza na kuunganisha Magari Tanzania cha GF Vehicles Assemblers (GFA), kilichopo Kibaha mkoani Pwani , kimesheherekea kufikia utengenezaji idadi ya magari 4000 tangu kilipoanza uzalishaji rasmi wa magari mwaka 2020. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endele).
Akizungumza wakati wa sherehe za kuruhusu gari ya 4000 kukanyaga aridhini baada ya kuunganishwa tayari kwa kutembea ,Meneja mkuu wa kiwanda hicho ,Ezra Mereng amesema wanaishukuru Serikali kupendekeza tozo ya maendeleo ya viwanda kwenye vichwa vya Terla za magari makubwa vinavyoagizwa nchini kwa asilimia 10 ili kuvilinda viwanda vya ndani na kuchochea ununuzi wa magari yalionunganishwa nchini.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa GFA, All Jawad Karmali amesema wamejipanga kuhakikisha wanaongeza mtaji katika uwekezaji ili kukabiliana na soko la Afrika mashariki na kati kwa upande wa magari.
Ameeleza kuwa wanataka kuifanya Tanzania kuwa nchi moja wapo inayounganisha magari na kulisha ukanda wote wa Afrika Mashariki kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyotengenezwa na Serikali.
Pia alizitaka tasisisi za serikali na kuagiza magari ambayo hayajaunganishwa ili kazi ya kuunganisha ifanyike na viwanda vya ndani kwa lengo la kukuza pato la Taifa na kuongeza ajira kwa watanzania, pia nchi kujipatia fedha za kigeni kwa kuuza magari yanayotoka Tanzania kwa nchi jirani.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uchangiaji Damu kwa kuendeleza mila ya Kimataifa ya Uwajibikaji wa Kijamii (CSR)
GSM kusambaza maji, vinywaji baridi kwa washiriki wa mbio za NBC Marathon
Je umejiunga?, weka pesa Meridianbet upate bonasi kubwa zaidi