June 17, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waziri Bashe amlipua Mpina mbele ya Rais

Hussein Bashe, Waziri wa KIlimo

 

VITA ya kutupiana maneno kati ya wanasiasa wawili Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) imebainika hadharani kwenye ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Simiyu. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainika leo tarehe 17 Juni 2025 ambapo Bashe, amesema kuwa wanasiasa waache kutumia zao la pamba kama siasa na kuongeza kuwa pamba ni zao la kuwatoa wakulima katika umaskini.

“Rais toka historia ya nchi hii, Mkulima wa Simiyu alikuwa anapata Kilo 200 hadi Kilo 300. Wanasiasa wa Mkoa wa Simiyu wameitumia Pamba kama siasa na sio zao la kiuchumi la kuwatoa watu katika umaskini.

“Kwanza hakuna mtu yoyote anayeweza kutathmini bei ya pamba isipokuwa serikali, hata wakiwa wanunuzi 500 kwenye Kijiji, bei ya pamba inaamuliwa na serikali. Na nimuombe Mpina hapa, mimi na yeye tulishakubaliana kuwa atasema hoja zake, nitazijibu hadharani,” alisema Bashe.

Bashe amesema Luaga Mpina, Mbunge wa Kisesa aliua kitalu cha mbegu kijiji cha Mwabisalu kwa siasa za kuwadanganya wananchi, serikali ikakiondoa.

“Kitalu kiliwekwa na wananchi wale walikuwa wanapata zaidi ya milioni 250-320, fedha za ziada ukiacha bei,” amesema Waziri Bashe.

Bashe akaongezea na kusema Mpina alienda kuhamasisha wapande mahindi katika hivyo vitalu badala ya Pamba.

“…Na mwaka 2019/20 alikuwepo kwenye serikali, ni mmoja kati ya watu waliompotosha Rais Magufuli kumwambia kuwa bei ya pamba duniani ni juu, Rais atangaze bei. Matokeo yake pamba ikafa,pamba zikanunuliwa 500 ikawa matatizo matupu”

“Nataka nimwambie yeye na wanasiasa wa Simiyu, sitaruhusu mtu yoyote aharibu mfumo ambao tumeanza kuujenga mwaka huu, Wilaya hii Rais Pamba ilianguka mpaka tani 30,000 tunatarajia kuvuna tani 60,000 na niwaambia wakulima endeleeni kukusanya pamba, bei inaamua serikali na tunapanga sisi bei, sio mtu yoyote,” amesema Bashe.

Amesema kuwa bei ya Pamba imepanda kutoka 1150 sasa kufikia 1200.

Tulianza na 1150, leo tupo 1200, mwaka jana tulianza 1150 tukamaliza na 1700. Serikali itakuwa inatoa bei kutokana na bei ya soko la dunia”

About The Author

error: Content is protected !!