
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaruhusu upande wa kukatisha ushahidi walioanza kutoa leo tarehe 16 Juni 2025 mpaka pale upande huo utakapomleta mahakamani hapo shahidi mtaalamu kwa ajili ya kuwa marejeo ya ushahidi ulianza kutolewa na Inspekta John. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 16 Juni na Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mhini. Na kueleza kuwa sheria inaruhusu kufanya hivyo.
Baada ya uamuzi huo Hakimu Mhini ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 1 Julai 2025.
Awali Nassoro Katuga Wakili wa Serikali Mwandamizi ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iahirishe shauri Na. 8606 la mwaka 2025 ili aje shahidi mwingine mahakamani ambaye ni mtaalamu wa uchunguzi wa video itakayotumiwa mahakamani hapo kama kielelezo.
Katuga aliyekuwa anamuungoza shahidi wa kwanza Inspekta John aliyejitambulisha kuwwa yeye ni mpelelezi wa makosa ya mtandaoni kwenye shauri leo tarehe 16 Juni 2025, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mhini.
Katuga alidai kuwa aruhusiwe shahidi huyo ili ushahidi wa kitaalam atakaoutoa uungane na ushahidi wa Inspekta John.
Ombi hilo limepigwa vikali na Wakili na Mpale Mpoki anayeongoza Jopo la mawakili wanaomtetea Lissu pamoja na Jeremiah Mtobesya na Peter Kibatala waliodai mahakamani hapo kuwa sheria hairuhusu utaratibu wa namna hiyo na kwamba wamriwe wamalize ushahidi wake.
Katuga akijibu hoja hizo amedaie kuwa mapingamizi ya utetezi imejichanga kwa kuwa kiongozi wao amedai hakuna kifungu cha kuahirisha “kwa upande mwingine wanakubali na wanasema mahakama itumie busara katika kutumia utashi wake kwenye kuamua hilo
“Wakili msomi mwenzetu Kibatala anakubali Kifungu cha 147 kwamba tumalize ushahidi wa shahidi huyu baadaye tumite lakini wamesahau kama kuna kifungu kidogo cha 5 …sasa tunalazimishwa kufunga ushahidi wetu hapa ili aulizwe umeleta video hapa sijaleta.”
Katuga amedai kuwa kila kesi inamuriwa kulingana na mazingira yake na itaendeshwa na mazingira yake…nature ya shauri hili tunazungumzia data za kumpyuta au ushahidi wa kieletroniki inayotaka kabla kielelezo hakijafika useme jinsi gani kilivyochakatwa unakizungumziaje kielelezo ambacho hakijapokelewa,” alidai Katuga.
Kibatala amedai kuwa kuruhusu suala la ushihidi liko kwenye mamlaka ya mahakama ‘sisi tunasisitiza kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuahirisha tukubaliane shahidi huyu ameletwa ili tusibishane kwani hajaletwa shahidi. Ni kilichowafanya wasimlete mtaalam na kuitoa video kama huyo shahidi anakuwa ni rejea ya shahidi huyu kwa hiyo kwa upande huo hatujaona hoja ya msingi”
Kibatala amesisitiza upande wa Jamhuri uamuriwe kufunga ushahidi wao “kwa mfano ushajua ushahidi wako utanguliwe na ushahidi wa Afisa ardhi kuna sababu zipi za kumtangulia kwa sababu shahidi anatakiwa atoe ushahidi wake amalize.”
Hakimu Mhini aliwauliza upande wa Jamhuri kwanini hawakujibu hoja ya kwanini hakuanza shahidi waliyemtaja kama ndio reference wa ushahidi wa Inspekta John.
Katuga amedai kuwa alishajibu kwamba mashauri yanaamuriwa kulingana na mazingira yake na kwamba msingi wa ushahidi huyo unajengwa na shahidi aliyetangulia.
ZINAZOFANANA
‘Polisi wanaiba kura’ ilivyomuibua shahidi wa serikali
Kesi ya Lissu shahidi wa kwanza wa Serikali aanza kutoa ushahidi wake
Lissu apewa muda kushauriana na mawakili wake kesi ya uchochezi