June 16, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Lissu : Nimewekwa kwenye mahabusu ya wanaosubiri kunyongwa

 

TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, juu ya kutotendewa haki kama mahabusu gerezani na kwamba amewekwa kwenye chumba cha waliohukumiwa kunyongwa (Death row) ilhali yeye ni mtuhumiwa. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu amedai hayo leo tarehe 16 Juni 2025, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Franco Kiswaga wakati shauri dhidi ya Uhaini Na. 8607 la mwaka 2025 likitajwa.

“Gereza la Ukonga kuna sehemu moja inaitwa ‘special room’ eneo maalum ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, mimi ninakaa hiyo sehemu wanayokaa wanaosubiri kunyongwa ‘death row.

“Sasa Mheshimwa ukiwa death row maana yake ni nini? kama ninachokaa mimi wakati sijahukumiwa kifo angalau bado sheria inasema wale waliohukumiwa kifo wanatakiwa watenganishwe na wafungwa wengine, mimi nimekaa death row tangu Ijumaa Kuu mpaka leo, na nikitoka kuonana na mawakili wangu au ndugu zangu ninaambatana na askari wawili muda wote kama inavyotakiwa kwa waliohukumiwa kifo,” alidai Lissu.

Hata hivyo upande wa Jamhuri umeeleza kuwa haujapewa nafasi ya kusikilizwa kutokana na madai hayo lakini Hakimu Kiswaga amesema kuwa madai hayo yamebainishwa na mshtakiwa kama taarifa hivyo itafanyiwa kazi kiutawala.

About The Author

error: Content is protected !!