June 16, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Lissu apewa muda kushauriana na mawakili wake kesi ya uchochezi

 

HAKIMU Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini anayesikiliza shauri Na. 8606 na uchochezi linamkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewapa muda wa nusu saa mawakili wa Lissu ili kuongea naye na kushauriana naye kuhusu mwenendo wa shauri . Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Awali wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga aliieleza mahakama hiyo kuwa tarehe 9 Juni 2025, mahakama hiyo iliamua juu ya maombi madogo Na. 13298 /2025 ya kuficha mashahidi ambao ni raia ambao sio askari na kwamba iwe sehemu ya mwenendo huo.

Mpale Mpoki, Wakili wa Lissu amedai mahakamani hapo kuwa kupata muda juu ya uamuzi huo ambapo aliomba muda wa nusu saa kwa ajili ya mashauriano na mteja wao (Lissu).

Hakimu Mhini aliyesikiliza shauri hilo alisema kuwa nusu saa ni nyingi.

Wakati huo huo, Lissu aliomba mahakamani hapo kupewa nusu saa kwa sababu ni muda wa siku 68 tangu ashikiliwe hajapata muda wa kuzungumza na mawakili wake kijadili masuala muhimu juu ya shauri hilo.

Hakimu Mhini ameahirisha shauri hilo mpaka saa sita na dakika 20 mchana.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online.

About The Author

error: Content is protected !!