June 14, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mmoja anusurika kwenye ajali ya Air India

 

VISHWASHKUMAR Ramesh raia wa Uingereza ameripotiwa kuwa ndiye mnusurika pekee wa ajali ya Air India iliyowaua watu takribani 241. Anaripoti Joyce Ndeki kwa msaada wa mitandao ya kimataifa … (endelea).

Ndege hiyo aina ya boeing 787 iliyokuwa ikielekea London ilianguka mda mfupi baada ya kuruka kutoka Ahmedabad magharibi mwa India.

Taarifa hiyo imetolewa na Malik Kamishna wa Polisi wa Ahmedabad ameliambia shirika la habari la India kuwa kulikuwa na mtu mmoja aliyenusurika ambaye alikuwa kwenye kiti namba 11A ya ndege hiyo ambapo yupo hospitalini na anaendelea na matibabu.

Vyombo vya habari vya India vilisema vilizungumza na Ramesh hospitalini na kumripoti akisema: “Sekunde thelathini baada ya kupaa, kulikuwa na kelele kubwa na kisha ndege ikaanguka. Yote yalitokea haraka.”

Kulikuwa na raia wa India 169, Waingereza 53, raia saba wa Ureno na raia wa Canada mmoja kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick, Air India ilisema

Ndege hiyo ilianguka kwenye makazi yaliyokuwa yakitumiwa na madaktari wanafunzi chini ya dakika moja baada ya kupaa na watu kadhaa waliokuwa karibu na eneo hilo wanahofiwa kufariki

Air India imethibitisha kuwa abiria wote wengine na wafanyakazi wa ndege wameaga dunia.

Familia kadhaa kutoka uingereza zimeripotiwa kufariki zikiwemo familia kutoka Londoni, Gloucester na Blackburn jamaa zao wameeleza huzuni kubwa na mshtuko waliopata.

About The Author

error: Content is protected !!