
SERIKALI katika kuhakikisha kuwa inatekeleza adhma yake ya matumizi ya nisgati safi ya kupikia sambamba kupunguza matumizi ya mafuta nchini imefuta kodia yab ongezeko la thamani (VAT) kwenye gasi asilia. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Akisoma bajeti Kuu ya serikali, Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha, amesema kuwa serikali imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye gesi asilia inayouzwa kwenda kwenye vituo vya kushindilia gesi (Compressed Natural Gas Stations) kwa ajili ya matumizi ya magari. Lengo la hatua hii ni kuweka unafuu kwa wawekezaji, kuvutia uwekezaji wa vituo vya 83 kusambazia gesi asilia iliyosindikwa kwenye magari na kupunguza utegemezi wa mafuta na uzalishaji wa hewa ya ukaa.
Dk. Nchemba amesema kuwa serikali itasamehe VAT kwenye mitungi ya gesi ya kupikia “serikali imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye matanki na mitungi ya gesi ya kupikia zinazotambulika kwa HS Code 7311.00.10 pamoja na mitambo ya kuondoa hewa ukaa yenye HS Code 8417.80.00 inayotumika katika uzalishaji wa mikaa mbadala”
“Hatua hii inalenga kupunguza gharama za upatikanaji wa bidhaa hizi ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh. 1,917.8 milioni,”amesema Dk. Nchemba.
Dk. Nchemba amesema kuwa serikali imefanya marekebisho kwenye kipengele cha 15 (8), cha Sehemu ya kwanza ya Jedwali la Misamaha ya Kodi ya ongezeko la thamani kwa kufuta neno Liquified Petroleum and Natural gases na kuweka neno Liquified Petroleum Gas.
Lengo la hatua hii ni kuweka ufafanuzi na kutatua changamoto zilizopo katika utoaji wa msamaha husika na hivyo kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mko vizur ila ongezen kuchambua kidogo. Habar ziko juu juu sana.