
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiw a kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa shule za Green Acres. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shule hizo, Jacklyne Siima Rushaigo, ilisema maadhimisho hayo yatafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 14 Juni 2025 katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre kuanzia saa 12 jioni.
Imesema Shule hizo zitakuwa zikiadhimisha miaka 25 ya Mafanikio Katika Sekta ya Elimu.
“Uongozi wa shule za Green Acres unapenda kuutarifu umma kuwa zinasherehekea miaka 25
tangu kuanzishwa kwake, ikiwa ni kipindi muhimu cha mafanikio, uuaji, na mchango mkubwa katika sekta ya elimu nchini Tanzania,” amesema.
Aidha, amesema shule hiyo inayojumuisha matawi mawili, moja likiwa Dar es Salaam (shule za awali, msingi na sekondari) na jingine Bunazi (awali na msingi) mkoani Kagera.
Amesema shule hizo zimekuwa vinara katika kutoa elimu bora kwa watoto na vijana, zikijivunia kuwa msingi wa malezi ya kizazi chenye maarifa, maadili na nidhamu.
“Katika kuadhimisha tukio hili adhimu, sherehe maalum ya kutimiza miaka 25 ya shule za Green Acres itafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 14 Juni 2025 katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre kuanzia saa 12 jioni,” amesema.
“Ushiriki wake ni heshima kubwa kwa familia ya Green Acres na ni uthibitisho wa mchango wa shule hizi katika maendeleo ya elimu nchini tunawakaribisha wazazi, walimu, wafanyakazi, wahitimu, marafiki na wadau wa elimu kushiriki katika tukio hili muhimu la kihistoria,” amesema Mkurugenzi.
ZINAZOFANANA
Aliyekataa uteuzi wa U-DC abwangwa uchaguzi wa CWT
Wanafunzi 214,141 wachaguliwa kidato cha tano, vyuo vya kati
Waziri Mkenda azindua Mashindano ya NBC ya Uandishi wa Insha, Wazo Bora la Biashara kwa wanafunzi