
Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere
SERIKALI imesema kuwa kiasi cha Sh. 11.16 trilioni zilitumika kulipa deni la serikali huku kiasi cha Sh.10.27 Trilioni ikitumika kulipa mishahara ya watumishi wa umma huku Sh. 741.5 Bilioni akitumika kuafanya maandalizi ya uchaguzi Mkuu na Sh. 1.01 Trilioni itumika kuwalipa wakandarasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hayo yameanishwa kwenye Bajeti inayowasilishwa bungeni leo tarehe 12 Juni 2025, na Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha.
Baadhi ya maeneo yaliyopelekewa fedha katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025 ni pamoja na: ugharamiaji wa deni la Serikali Sh. 11.16 trilioni, ugharamiaji wa mishahara ya watumishi wa umma Sh. 10.27 trilioni, na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Sh. 741.4 bilioni.
Aidha, kwa kutambua mchango wa wakandarasi, wazabuni na watoa huduma katika kujenga Taifa, Serikali imeendelea kulipa madeni yaliyohakikiwa ambapo kiasi cha Sh. 1.01 trilioni kimelipwa. Ulipaji wa madeni haya umesaidia kulinda mitaji na kuchochea shughuli za kiuchumi nchini.
“Serikali imeendelea kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikijumuisha: Ujenzi wa barabara, madaraja, na viwanja vya ndege ambapo Sh. 1.58 trilioni zilitolewa, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya reli ikiwemo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) Sh. 1.68 trilioni, utekelezaji wa mradi wa Kufua Umeme katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) MW 2,115 na mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Sh. 574.8 bilioni,” amesema Waziri Mwigulu.
Amesema kuwa kisia cha Sh. 179.8 bilioni, kimetumika katikaa ujenzi na ukarabati wa viwanja vya mpira kwa ajili ya maandalizi ya AFCON 2027 .
“Serikali pia imeendelea kuboresha huduma za jamii kwa kugharamia: mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na vyuo vya kati ambapo Sh. 636 bilioni, zimetolewa; Programu ya Elimumsingi na Sekondari bila Ada Sh. 444.7 bilioni, miradi ya maji mijini na vijijini Sh. 378.7 bilioni, ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwa ajili ya hospitali za mikoa, kanda na rufaa Sh. 414.7 bilioni, ujenzi na ukarabati wa hospitali za wilaya, mikoa, kanda na rufaa Sh. 47.2 bilioni na ujenzi wa vituo vya afya na zahanati Sh. 7.3 bilioni.
ZINAZOFANANA
Mmoja anusurika kwenye ajali ya Air India
Kicheko kwa watumiaji gesi za kupikia
Bajeti ya mwaka 2025/2026 trilioni 56.49