June 11, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Serikali yaanza vibaya kesi ya Gwajima, pingamizi lao latupwa

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali pingamizi la serikali kwenye shauri Na. 13189 ya mwaka 2025 iliyofinguliwa na Bodi ya wadhamini ya kanisa Glory of Christ Tanzania Church imefungua shauri katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ikipinga hatua ya msajili jumuia za kiraia kufuta usajili wa kanisa hilo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo imefunguliwa tarehe 4 Juni 2025, ambapo imefunguliwa kwa hati ya dharura waombaji wakiomba kusimamishwa utekelezaji wa agizo la kufungwa kwa kanisa hilo mpaka pale shauri la msingi litakapokamilika.

Waombaji wanaitaka mahakama iwape haki yao ya kikatiba ya kufanya ibada na kusanyiko la kuabudu.

Katika maombi hayo Kanisa hilo linaloongwa na Askofu Josephat Gwajima linawakilishwa na Wakili Peter Kibatala huku wajibu maombi wakiwa Msajili wa Jumuiya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP.

Wakili Vivian Method aliyeongoza jopo la mawakili wa serikali aliwasilisha pingamizi mahakamani kwamba barua inayolalamikiwa ya kufungia kanisa hilo inataja jina la Glory of Christ Church na sio The Registered Trustees of Glory of Christ Tanzania Church na kuitaka mahakama kulitupilia mbali shauri hilo kwa kuwa linahusu hisia na uhalisia.

Kibatala alipinga hoja hizo kwa kueleza kuwa tayari Polisi wawemazuia waumini kuendelea na ibada ikiwa ni wazi haki zao zimepokwa.

Baada ya mabishano ya pande zote Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo Dk. Juliana Masabo alitupilia mbali pingamizi la serikali na kutaka shauri hilo lisirihusiwe kufunguliwe.

About The Author

error: Content is protected !!