
TAASISI ya Haki za Wasanii Tanzania (TARO), imeendesha kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kujadili marekebisho ya Sheria ya Sanaa ya Taifa Na. 23 ya 1984. Kikao hicho kilifanyika Dodoma kililenga kushughulikia mapungufu ya sheria ili kuongeza chachu ya ukuaji wa sekta ya utamaduni nchini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Katika kikao hicho mada kuu zilizojadili wa ni Pamoja na malipo ya ada na vibali kwa wasanii na wadau, adhabu kwa wasanii wasiosajiliwa, udhibiti wa maudhui ya sanaa, usawa wa kijinsia kwenye sekta ya sanaa na utamaduni masuala mbalimbali ya ustawi wa sanaa nchini ikiwamo matumizi ya mtandao na sanaa za kidigitali kama akili mnembo (AI), uhalisia pepe (Virtual Reality) na pesa za mtandaoni.
Aidha kikao hicho Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilikiri mapungufu ya sheria hiyo sana ana marekebisho yanahitaji mjadala mpana baina ya wadau, serikali na Kamati za Bunge.
Hata hivyo Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeshauri kwa kuwa uchaguzi unakaribia na Bunge halitaweza kufanya mabadiliko kwa haraka, ni vyema TARO kusubiri na kupisha kwanza vuguvugu la uchanguzi. Na mazungumzo zaidi yafanyike na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Marekebisho ya Sheria, na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Kwa upande wake TARO wamesema “Wasanii ndio robo ya utamaduni wetu, marekebisho haya yanalenga kulinda haki zao na kuleta mazingira mazuri kwa sekta hii. Tunawataka wadau wote kushirikiana.”
Ikumbukwe taasisi ya kutetea haki za wasanii (TARO) imekua ikitetea wasanii kwa takribani miaka 3 sasa.
ZINAZOFANANA
Wazazi wahusiwa kutowalaza watoto wa jinsia tofauti chumba kimoja
Wanafunzi 214,141 wachaguliwa kidato cha tano, vyuo vya kati
Mahakama ya Rufaa yasisitiza Mchechu kulipwa Bili 2.5