
DOROTHY Semu, Kiongozi wa Cham cha ACT Wazalendo ameongoza viongozi na makada wa chama hicho kumkaribisha na kumpokea Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyejiunga rasmi na chama hicho. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Hafla hiyo ya ukaribisho imefanyika leo 5 Juni 2025, kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, jijini Dar es Salaam, Dorothy Semu amemtaja kiongozi huyo wa kiimani ambaye ni pia mwanaharakati wa muda mrefu kuwa ni ‘Mwamba wa Harakati’
Naye Sheikh Ponda akizungumza kwenye hafla hiyo, amesema ameona umuhimu wa kujiunga na oparesheni ya chama cha ACT Wazalendo ili kulinda demokrasia inayolenga kurejesha haki, uwazi na usawa katika michakato ya uchaguzi.
“Sheria inapaswa kuwa chombo ya kulinda binadamu siyo kutesa wananchi Tatizo la nchi yetu halina utawala wa kizalendo unaoangalia maslahi ya umma na wala hauzingatii sheria,” alisema Sheikh Ponda.
Pia ametoa wito kwa vijana wanawake wazee na viongozi wa dini kuungana katika uwanja wa mapambano wa kudai haki za kisiasa kuhakikisha kura zinahesabiwa kwa haki ili kupata viongozi wanaokidhi haja za wananchi.
ZINAZOFANANA
Wanafunzi 214,141 wachaguliwa kidato cha tano, vyuo vya kati
Chaumma waeleza sababu za Chopa kuota mbawa
Padre Kitima aadhimisha misa ya shukrani