June 6, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bei ya Petroli, Dizeli yashuka mwezi Juni

 

MAMLAKA ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Juni 2025. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Hali hiyo imechangiwa na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia pamoja na mabadiliko kwenye gharama za uagizaji na usafirishaji.

EWURA imetangaza kuwa Bei za mafuta yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa shilingi 72.16, kwa petroli na kwa Sh. 72.16, kw dizeli kwa Sh. 51.89, na mafuta ya taa kwa Sh 184.93 kwa kila lita huku Bandari ya Tanga imeshuhudia punguzo la Sh 69.41 kwa petroli na Sh 50.10 kwa dizeli, huku Mtwara bei ya petroli ikipungua kwa Sh 71.65 na dizeli kwa Sh 51.37.

Takwimu za miezi mitatu mfululizo — Aprili, Mei na Juni 2025 — zinaonesha mserereko wa kupungua kwa bei. Petroli katika bandari ya Dar es Salaam imeshuka kutoka Sh 2,905.34 (Aprili) hadi Sh 2,684.54 (Juni), tofauti ya Sh 220.80. Tanga bei imepungua kutoka Sh 2,904.93 hadi Sh 2,750.34, na Mtwara kutoka Sh 2,811.36 hadi Sh 2,750.34 — punguzo la Sh 61.02.

Kwa upande wa dizeli, Dar es Salaam imeshuka kwa Sh 60.17, Tanga kwa Sh 115.25, na Mtwara kwa Sh 119.97 ndani ya kipindi hicho hicho. Mafuta ya taa pia yameshuka kwa asilimia 3.7 katika soko la dunia, hali iliyochangia bei nafuu nchini.

Punguzo hilo limeakisi kupungua kwa bei ya mafuta kimataifa kwa asilimia 0.9 (petroli), asilimia 3.4 (dizeli), na asilimia 3.7 (taa). Aidha, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa asilimia 0.63, japokuwa gharama za kuagiza mafuta zimeongezeka kwa asilimia 4.34 (petroli), 22.43 (dizeli) katika bandari ya Dar es Salaam, huku mafuta ya taa yakishuhudia upungufu wa asilimia 1.65. Mtwara, gharama za uagizaji waeď petroli zimepanda kwa asilimia 51.55 na hakuna mabadiliko kwa dizeli.

EWURA imefafanua kuwa ukokotoaji wa bei kikomo kwa Juni 2025 umetumia viwango vipya vya usafirishaji vilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 5083 la tarehe 25 Aprili 2025,viwango hivyo vimeanza kutumika rasmi leo nchini kote.

About The Author

error: Content is protected !!