June 5, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chaumma waeleza sababu za Chopa kuota mbawa

 

CHAMA cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kupitia Katibu wake Mkuu Salum Mwalimu, kimetoa sababu ya kushindwa kutua na Helkopta (Chopa) kwenye uzinduziwa Operesheni Chaumma For Change jijini Mwanza (C4C). Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea)

Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 03 Juni 2025, kwenye viwanja vya Furahisha, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao, Hashim Rungwe.

Akitolea ufafanunuzi huo Salum Mwalimu, ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama hicho alisema kuwa, hapo awali walifanikiwa kupata Helikopta kutoka kwenye moja ya makampuni ndani ya nchi, lakini changamoto ya vibali kutoka kwenye mamlaka ya Anga ilikwamishwa jambo hilo kutokana na kufanyika kwa ukaguzi wa chopa zote ambazo zimesajiliwa Tanzania.

“Tarehe 4 nilifanya mawasiliano na kampuni moja ya Air Con Service Ltd kwa ajili ya kutuletea ndege, mipango hii hatujaianza jana, tulianza mwezi mmoja uliopita, kampuni ile tukiwa Katikati ya mazungumzo, ilitoka tangazo kutoka kwenye mamlaka za anga Tanzania kuzuia shughuli zote za urukaji wa Helikopta zenye usajili wa Tanzania,” alisema kiongozi huyo.

Aidha Mwalimu alisema kuwa, mara baada ya kushindikana kupata chopa kupitia kampuni za ndani, walifanya utaratibu na kufanikiwa ndege nyingine kutoka Afrika Kusini lakini ilikuwepo nchini Uganda, lakini nayo iliota mbawa kutokana na kukatika kwa mawasiliano na wamiliki.

“Wakatutafutia Helikopta kutoka Afrika Kusini ambayo ipo Uganda, wakasema wakimaliza Uganda watakuja kutupa huduma, kwa kuwa helikopta kutoka nje hazikuwa zimezuiliwa lakini mwisho wa siku wakawa hawapatikani na hivyo tukaamua kutafuta ndege nyingine.

“Tulipata ndege kutoka Kenya, mara baada ya vibali kukamilika ilichelewa kuruka kutokana na giza, na hivyo kesho majira ya saa 1 asubuhi ndege itakuwa imewasili Mwanza,” alisema Mwalimu.

Chama hicho kinafanya Operesheni yake ya kwanza, toka kilipopata uongozi mpya ambao walikuwa wanachama waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambao walijiondoa kwenye chama hicho mara baada yauongozi mpya chini ya Tundu Lissu kuingia madarakani.

About The Author

error: Content is protected !!