
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imempogeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kufutia tuzo maalum ya heshima aliyotunukiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuthamini kazi kubwa na nzuri aliyofanya katika kuleta maendeleo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Aidha, benki hiyo imeahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa kuendeleza ushirikiano wake na serikali pamoja sekta binafsi katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa kwa manufaa ya Watanzania kupitia huduma bora za kifedha.
Akizungumzia tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi aliyekuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, pamoja na kumpongeza Rais Samia kwa tuzo hiyo alisema benki ya NBC inaunga mkono mafanikio hayo kwa kuendelea kubuni na kutoa huduma mbalimbali za kifedha ikiwemo mikopo na ufadhili wa miradi mbalimbali ya kimkakati.
“Tunampongeza Rais Samia kwa tuzo hii ya heshima inayoashiria kwamba jitihada zake katika kuchochea kasi ya maendeleo hapa nchini inaonekana na inathaminiwa pia na miimili mingine ya kitaifa. Katika kuunga mkono mafanikio haya NBC tunaahidi jitihada zaidi kwa kutoa kipaumbele kwenye kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, sekta ya kilimo, afya, elimu, utalii, michezo na sekta nyingine muhimu,’’ alitaja.
Sabi alitolea mfano jitihada za benki hiyo ikiwa kama mtaalam mshauri katika kufanikisha uuzwaji wa hati fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga-UWASA) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji mkoani Tanga mwaka jana.
“Huo ni mfano mmoja tu kati ya mifano mingi ya miradi tunayoshiriki kuifanikisha kupitia mikopo mbalimbali kwa serikali na wazabuni, ufanikishaji wa miamala ya kifedha ikiwemo ya kimataifa, kubadili fedha za kigeni pamoja na ufadhili wetu kwenye jitihada za kijamii hususani kwenye sekta ya afya,’’ alisema Sabi.
ZINAZOFANANA
Shinda Samsung A25 Mpya kwa kucheza Super Heli na Meridianbet
Magari ya umeme na gesi kutengenezwa nchini
Tangaza vita ya bahati! Shinda na ndani ya kasino na 3 Oaks