May 31, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kilatu: Msajili wa vyama anaupendeleo

 

HATUA ya Msajili wa vyama vya siasa kutowatambua wajumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walioteuliwa na Baraza kuu la chama hicho tarehe 21 Januari 2025, jijini Dar es Salaam, imeibua mjadala wa kitendo hicho kimelenga wapinzani pekee yao. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kutowatambua viongozi hao akiwemo John Mnyika Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Rugemaliza Nshala Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Godbless Lema Mjumbe wa Kamati Kuu na wengine amefuta ruzuku ya chama hicho akidai haina uongozi utakaosimamia fedha za umma.

Leo tarehe 30 Juni 2025, Edson Kilatu wakili wa kujitegemea akizungumza na Jambo TV, amesema kuwa ulezi wa Msajili wa vyama vya siasa unauelekeo wa upendeleo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia amesema ofisi ya msajili wa vyama vya siasa namna ya uongozi wake ni wa kufikilika kwa kuwa linapotokea suala la vyama vingine ndipo inajitokeza kukemea au kurekebisha ila chama tawala ikikosea hawaonekani wakisema kitu hivyo haiwezwi kuachwa ikajiongoza yenyewe.

“Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ije iseme ni kifungu gani cha sheria kipo kinachosema ana mamlaka ya kutengua uteuzi wa viongozi ndani ya chama.”

Kifungu kilichopo ni kufuta chama ila sio kutengua uteuzi wa uongozi ndani ya chama sheria ilijua hiyo ni mfumo wa ndani ya chama hausiani na ofisi ya msajili.

Amesema, “hiyo sheria ya msajili wa vyama vya siasa iangaliwe upya na pengine nafasi isikae kwenye sheria ya vyama vya siasa pekee iwe ni nafasi ya kikatiba kwa sababu mtu mwenye uwezo wa kuathiri uhuru wa watu kujumuika, kufuta vyama na uteuzi wake ni jambo la hatari wasije kufuta vyama vyote wakabakisha chama kimoja.”

About The Author

error: Content is protected !!