
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza kuwa mechi ya pili ya fainali ya kombe la Shirikisho kati ya Simba na RS Berkane ya Morroco itafanyika katika uwanja wa Aman visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mechi hiyo ilipangwa kufanyika katika uwanja Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambao uko kwenye ukarabati.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Caf, Veron Mosengo, imebainisha kuwa uamuzi huo unatokana na ushauri wa kitaalamu waliopatiwa hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea nchi.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanatambua jitihada za serikali na wadau mbalimbali katika kushughulikia ukarabati wa ‘Mkapa’ lakini mechi hiyo itapigwa uwanja wa Aman hivyo waendelee na maandalizi kwenye uwanja huo.
ZINAZOFANANA
Suzan Kiwanga ang’oka Chadema na wengine 50
Msajili atengua uteuzi wa viongozi wa Chadema
Meridianbet inakupatia mpunga wa maana leo