
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa
JESHI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeleza sababu za kumkamata Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Amani Golugwa. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Faustine Mafwele amesema saa 06:45 usiku tarehe 13 Mei 2025, katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lango namba 03 (terminal 03) lilimkamata Golugwa kwa kuwa alikuwa na tabia ya kutoka nje ya nchi bila kufuata utaratibu.
“Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa nchini,” alisema Mafwele.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuhusu suala hilo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu Mtajwa.
ZINAZOFANANA
Msajili Hazina: Ni wakati wa Tanzania kunadi fursa za uwekezaji kimataifa
Dk. Doriye awavisha vyeo vya kijeshi Maafisa 145 na askari 476 wa NCAA
Hospitali ya Mt. Joseph Peremiho yatoa nafuu mikoa ya Kusini