
Ikiwa ni Jumamosi nyingine ya kijanja, wakali wa ubashiri Meridianbet leo hii wamefika Mbezi Africana pale Kituoni na kufanya zoezi la usafi. Lakini pia leo hii mitanange kibao inaendelea hivyo nafasi ya wewe kuibuka bingwa ni kubwa.
Kampuni ya Meridianbet kupitia timu yake ya Uwajibikaji wa Kijamii (CSR) Tanzania imefanya zoezi la usafi katika kituo cha mabasi cha Africana Stendi, kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, Mheshimiwa Anna Lukindo, ofisi yake pamoja na wananchi wa eneo hilo.
Zoezi hili limehusisha usafishaji wa mazingira ya stendi, ukusanyaji wa taka na utoaji wa vifaa maalum vya usafi kama mifuko, glovu, na maji kwa washiriki, huku likilenga kuhamasisha usafi wa mazingira na mshikamano kati ya sekta binafsi, uongozi wa eneo, na jamii.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwakilishi wa Meridianbet alisema: “Kama sehemu ya jamii, tunawajibika kulinda afya ya watu wetu kwa kuhakikisha maeneo ya umma yanakuwa safi na salama. Usafi ni afya, na afya ni maisha hii ndiyo sababu kubwa iliyotufanya kuchukua hatua hii ya kijamii.”
Mpango wa Kimataifa wa Usafi – Ushirikiano wa Tanzania na Serbia
Zoezi hili limefanyika kwa wakati mmoja na shughuli nyingine kama hiyo nchini Serbia, ambako Timu ya CSR ya Meridianbet Serbia imefanya usafi katika hifadhi ya Fruška Gora, sambamba na udhamini wa mbio za EPIC MTB.
Pia leo hii unaweza ukatusua kijanja na Meridianbet kwani mechi kibao zipo uwanjani .Suka jamvi lako la ushindi leo na ubashiri hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.
Kwa kufanya zoezi hili kwa pamoja, Meridianbet Tanzania imeungana rasmi na timu ya kimataifa ya Meridianbet katika kutekeleza mpango wa Usafi wa Kimataifa, ukiwa ni sehemu ya dhamira ya kampuni ya kulinda mazingira na kuchangia maendeleo endelevu katika maeneo yote tunayofanya kazi.
Kupitia kampeni hii, Meridianbet inatoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira na kuendeleza ushirikiano kati ya mashirika, viongozi wa serikali, na wananchi kwa ujumla.
Zaidi ya mifagio, mapipa ya taka na vifaa vya usafi kutolewa, Meridianbet pia ilitoa elimu kwa wahudumu wa stendi na abiria juu ya umuhimu wa kutunza mazingira wanayoyatumia kila siku.
Kwa Meridianbet, CSR si tukio bali ni mtazamo endelevu wa kuwainua na kuwahudumia Watanzania. kampuni hii imeendelea kuthibitisha kwamba mafanikio ya kibiashara yanapokuwa sambamba na huduma kwa jamii, ndipo maana halisi ya maendeleo jumuishi inapatikana.
ZINAZOFANANA
Furahia unapocheza kasino ya mtandaoni kwa sloti hii
Vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi vyaongezwa
Serikali kuongeza thamani ya madini