
MKURUGENZI wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Dk. Rashid Mfaume amezielekeza timu za usimamizi wa Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) na ngazi ya Halmashauri (CHMT) kusikiliza kero na maoni kutoka kwa wananchi pindi wanapotembelea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwaajili ya ziara za kikazi na ukaguzi. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Dk. Mfaume amesema hayo alipotembelea Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kukagua upatikanaji wa huduma za afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Katika Manispaa hiyo.
“Mara nyingi RHMT na CHMT tumekuwa tukifanya ziara za ukaguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya bila kusikiliza mrejesho wowote kutoka kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa ziara hizo,” amesema Dk. Mfaume.
Amesema tusipopita na kusikiliza kero au maoni ya wananchi namna wanavyopokea huduma, uwekezaji wote ambao serikali umefanya katika ujenzi wa vituo vya afya, hospital na zahanati utakuwa hauna maana hivyo ni muhimu sana kuwasikiliza wananchi.
Aidha, Dk. Mfaume amevielekeza vituo vya kutolea huduma za afya kwa kushirikiana na CHMT kutumia vizuri vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) katika kutangaza huduma zinazotolewa na vituo hivyo.
“Kuna huduma nyingi kubwa na muhimu sana ambazo hivi sasa Nchini zinatolewa hadi ngazi ya vituo vya afya lakini wananchi wetu hawana taarifa hivyo ni muhimu vituo na halmashauri kutumia wataalamu wetu katika vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) kutangaza huduma hizo kwa Wananchi,” amesisitiza.
ZINAZOFANANA
Serikali kukarabati vituo konhwe vya huduma ya afya
Mil 800 kugharamia matibabu ya macho Siha
Dar yatakiwa kujenga vituo vya Afya jwa ghorofa