
KUNDI la watia nia 55 wa ubunge maarufu kama G55 wametangaza kujiondoa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na malalamiko ya chama kukosa usawa. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Wamesema hayo leo tarehe 7 Mei 2025, kwenye mkutano wa waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Benson Kigaila, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania-Bara alitangaza uamuzi huo huku akieleza chama hicho kimekiuka misingi ya uanzishwaji wake.
“…baada ya kugundua hawa jamaa wanakokwenda hawana nia njema na chama na kwamba hawa jamaa watakiua hiki chama tumeona hiki chama kisife mbele yetu tukasingiziwa kwamba na sisi tulikuwa sehemu ya kukiua hiki chama.”
Kigaila ametoa rai kwa wanachadema wengine waliohisi kubaguliwa kushuka kwenye jahazi hilo. “Nawashauri WanaChadema wanaobaguliwa, wanaoumizwa na mambo yanayoendelea tusiwe sehemu na tusiwape sababu kwamba hiki chama kimekufa hawa wapo kwa sababu timu mbowe ipo.”
Kigaila amesema kuwa G55 wameadhimia kuondoka kwenye chama hicho kwa pamoja. “Sisi tumeamua wote pamoja tumejiondoa Chadema hatuwezi kuwa na chama ambacho maamuzi yake hayatokani na vikao, Katiba haifuatwi tuliingia Chadema kwa sababu ya malengo na tunajitoa Chadema kwa sababu Chadema imeachana na malengo yalioyotufanya tuingie.”
Amesema pia, “Sisi tunatafuta jukwaa muafaka la kwenda kutumikia watanzania kwa sababu hatujazeeka, tunaondoka Chadema tunakwenda kutafakari tunaenda chama gani,lakini naomba mfahamu CCM sio mbadala wetu.”
ZINAZOFANANA
Samia amteua Twange kuwa bosi Tanesco, ahamisha ma-DC wanne
Mahakama yaiamuru Serikali kumfikisha Lissu mahakamani
Serikali itachukua hatua kwa waliomshambulia Padri Kitima