
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imeungana na maelfu ya wafanyakazi kote nchini kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, MEI Mosi ambayo kitaifa yamefanyika kwenye Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida, yakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).
Maadhimisho hayo yaliyohusisha wafanyakazi na viongozi wengine waandamizi akiwemo Dk. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete yaliratibiwa na Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyama mbalimbali vya wafanyakazi. Benki ya NBC imeendelea kuwa moja ya wadhamini muhimu wa na maadhimisho hayo.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kusherehekea siku hiyo muhimu akiwemo Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC Miraji Msuya na Meneja wa NBC tawi la Singida, David Mushi
Semunyu alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye maadhimisho hayo unatokana na kutambua umuhimu wa siku hiyo kwa wafanyakazi ambao ni nguzo muhimu katika ustawi wa Uchumi wa nchini huku benki hiyo ikichangia ukuaji huo kupitia huduma mbalimbali za kibenki inazozitoa kwa wafanyakazi hao na serikali kwa ujumla.
“Katika maadhimisho haya NBC tunaungana na maelfu ya wafanyakazi wenzetu kote nchini kusheherekea siku hii muhimu sana kwetu sote, kwanza tukiwa kama wafanyakazi, pili tukiwa wadhamini muhimu katika kufanikisha uratibu wa maadhimisho haya na tatu tukiwa kama watoa huduma za kifedha kwa wafanyakazi kupitia matawi yetu yaliyopo kote nchini ikiwemo hapa Singida pamoja na maelfu ya mawakala wetu kote nchini,’’ alisema.
Kwa mujibu wa Semunyu, ushirikiano wa benki hiyo na wafanyakazi unaimarishwa zaidi kupitia huduma za benki hiyo zinazotolewa kwa kundi hilo kwa kuzingatia mahitaji yao ikiwemo kuwatunzia amana zao kupitia akaunti mbalimbali kulingana na machaguo yao.
“Pia tunawapatia mikopo ya muda mrefu na muda mfupi bila dhamana na mikopo hiyo imekuwa na tija sana kwao kwa kuwa inawawezesha kujenga au kununua nyumba, kununua magari na vitendea kazi mbalimbali. Yote hayo wanaweza kuyafanya kwa urahisi zaidi kupitia huduma zetu zilizorahishwa kidigitali yaani ‘NBC Kiganjani’. Ni kupitia urahisishwaji huu wa huduma ndio maana tunasema NBC Kiganjani, Ukigusa Tu Imooo,’’ alisema.
Zaidi Semunyu alitumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wengine wa benki ya NBC kwa namna wanavyotimiza majukumu yao kwa weledi, ubunifu na ufanisi wa hali ya juu hatua ambayo imekuwa ikiwavutia zaidi wateja wa benki hiyo wakiwemo wafanyakazi wa mashirika na taasisi mbalimbali wanaoitazama benki hiyo kama kimbilio muhimu katika huduma za kifedha.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Meneja wa NBC Tawi la Singida, David Mushi alisema katika kuwafikia zaidi wananchi wakiwemo wafanyakazi mkoani humo, benki hiyo pamoja na kuwekeza zaidi kwenye huduma za kidigitali imeendeleza kushirikiana zaidi na mawakala wa huduma za kibenki mkoani Singida ambapo kwa sasa benki hiyo ina jumla ya mawakala 300 mkoani humo.
Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya pamoja na mambo mengine aliwasilisha shukrani zake za dhati kwa taasisi fedha na wadau wengine ikiwemo benki ya NBC kwa jitihada zao katika kufanikisha maadhimisho huku akionesha kuguswa na mchango unaotolewa na taasisi hizo katika kuwahudumia wafanyakazi hao.
ZINAZOFANANA
Mwanza mbioni kuzalisha vyanzo vipya vikubwa vya kodi
Shinda simu mpya ya kisasa na MERIDIANBET!
Shinda mamilioni kwa kucheza kasino na sloti ya Sticky 777.