
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Amend Tanzania, imezindua awamu ya pili ya kampeni yake ya Usalama Barabarani inayojulikana kama ‘Be Road Safe Africa’. Mpango huu wenye kuleta mageuzi kwa usalama barabarani unalenga kuwawezesha watoto na kuboresha uelewa wa usalama barabarani katika jamii zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Awamu ya pili itaendeleza jitihada zake katika shule za msingi zingine tano ambazo ni: Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), and Salasala (Salasala).
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), duniani kote, majeraha ya barabarani ndio chanzo kikuu cha vifo kwa vijana wa umri kati ya miaka 10 na 19, pia ni chanzo cha tatu cha sababu zinachopelekea ulemavu wa maisha katika kundi hili, na vilevile chanzo cha tatu cha sababu zinazopelekea vifo kwa watoto wa miaka mitano mpaka tisa. Mbali na kusababisha kifo na ulemavu, majeraha ya barabarani yanaweza kuwa na athari za kudumu kwa watoto kutokana na mfadhaiko na msongo wa mawazo, kukatiza masomo, na kusababisha matatizo ya kiuchumi nyumbani kutokana na gharama kubwa za matibabu.
Katika vifo 31 kwa kila watu 100,000, WHO inaripoti kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini Tanzania ni karibu mara 1.7 ya kiwango cha kimataifa na juu zaidi ya wastani wa Afrika.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda, aliongoza uzinduzi huo, akisisitiza dhamira ya serikali ya kupunguza ajali za barabarani zinazosababisha vifo vya maelfu ya watu kila mwaka.
“Ajali za barabarani zimeendelea kuwa changamoto kubwa nchini Tanzania. Kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inaenda sambamba na jitihada zinazoendelea za serikali katika kuhimiza shughuli za usalama barabarani. Takwimu za Jeshi la Polisi Tanzania zinaonyesha kuwa mwaka 2024 pekee, nchi ilirekodi ajali 1,735 za barabarani ambapo ajali 1,198 kati ya hizo zilisababisha vifo vya Watu 1,715.
“Makosa ya kibinadamu, ikiwemo kupuuzia alama za barabarani, kuendesha gari kwa uzembe, na mwendokasi, vilichangia 97% ya matukio haya. Tunahimiza sekta binafsi na wadau wa usalama barabarani kuendelea kushirikiana na serikali kuelimisha na kuongeza uelewa kuhusu usalama barabarani,” alisema SACP Mkonda.
Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Puma Energy Tanzania, Mhandisi Lameck Hiliyai, amesisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kulinda usalama na ustawi wa jamii: “Kwetu Puma Energy, usalama ndio msingi wa uendeshaji wa shughuli zetu. Kupitia mpango huu, tunatekeleza adhma yetu ya kuzingatia na kusimamia misingi ya afya, usalama, ulinzi, na mazingira (HSSE) kuhakiksha watoto, ambao ndiyo kundi hatarishi zaidi la watumiaji wa barabara, wanawezeshwa na elimu ya kuwa salama. ‘Be Road Safe Africa’ inaboresha usalama wa watoto wa shule za msingi kupitia programu za elimu zinazowawezesha kuwa watumiaji wa barabara wanaowajibika.”
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda ameipongeza Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa jitihada zake za kutoa elimu ya usalama barabarani. “Watoto wanaosoma shule zilizo karibu na barabara wako hatarini zaidi.
Amesema tunashukuru mpango huu na tutaendelea kushirikiana na Puma Energy ili kupanua wigo wa kampeni hii kote nchini. Pia tunatoa wito kwa makampuni mengine kuungana ili kuhamasisha usalama barabarani, kwani mafanikio ya biashara zao yanategemea afya na ustawi wa jamii wanazozihudumia”.
Kupitia shughuli wanazozifurahia na kuzipenda, tunawafundisha watoto kuhusu usalama barabarani na kuwahimiza kueneza ujumbe katika jamii zao. Mojawapo ya shughuli ya kuvutia zaidi katika programu hii ‘Mahakama ya Watoto’, ambapo watoto huchukua jukumu la ‘majaji wa usalama barabarani’ na kusaidia kuwawajibisha madereva kwa matendo yao ya barabarani.
Puma Energy Tanzania inashirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Amend Tanzania na washirika wengine wa ndani wakiwemo mabaraza ya usalama na polisi kufanikisha kampeni hii.
Awamu ya kwanza ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’, ilitekelezwa mwaka 2023 and 2024, ambapo iliwafikia watoto zaidi ya 38,000 katika shule 20 za nchini Tanzania, Botswana, Zambia, na Zimbabwe. Awamu ya pili itatekelezwa katika nchi za Tanzania, Botswana, Zambia, Zimbabwe, na Afrika ya Kusini.
ZINAZOFANANA
Watanzania wahimiza kufanya mazoezi kwa Afya
Waziri Masauni aelezea mafanikio ya Muungano
Ofisi ya Msajili Hazina yaendesha mafunzo kwa kamati za bunge