
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel
NAIBU Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema, amesema serikali imeongeza vituo vya Dialysis katika hospitali 15 za rufaa za mikoa na hospitali zote za kanda hapa nchini ili kusogeza karibu huduma ya usafishaji wa figo na kupunguza gharama za matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Amesema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2025 wakati akijibu swali la mbunge wa Mbulu Mjini, Isaay Zacharia aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kupunguza gharama za usafishaji figo katika hospitali za umma.
“Vilevile serikali itaongeza wadau na taasisi zinazo ingiza vitenganishi, vifaa tiba na dawa zitumikazo badala yakuacha mtu mmoja au Taasisi kutawala soko bila kuruhusu ushindani pia kuhamasisha viwanda na ubunifu ndani ya nchi,” amesema Mollel.
Pamoja na hayo Mollel amesema serikali imesambaza kwenye hospitali za Rufaa za mikoa nchini mashine zaidi ya 100 pamoja na vitendanishi vyake hatua inayolenga kuondoa mzigo wa gharama kubwa kwa wagonjwa wa figo na kuwawezesha kupata huduma kwa urahisi zaidi katika maeneo yao ya karibu.
Aidha, ametoa rai kwa wananchi kwamba mara utekelezaji wa bima ya afya utakapoanza wajiunge mara moja kwani itakuwa ndio njia pekee ya kuwasaidia kuepukana na gharama za matibabu.
ZINAZOFANANA
Serikali kukarabati vituo konhwe vya huduma ya afya
RHMT na CHMT sikilizeni kesro, maoni kutoka kwa wananchi – Dk. Mfaume
Mil 800 kugharamia matibabu ya macho Siha