
TAASISI ya kifedha ya EFTA na GSM zimeungana kwa kusaini mkataba wa makubaliano ya kuwakopesha wakulima na wafanyabiasha wadogo na kati kwa kuwawezesha kupata mikopo ya vitendea kazi kulingana na shughuli zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 8, 2025 jijini Dar es Salaam ambapo ni muendelezo taasisi hiyo katika kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi nchini, kuwawezesha vifaa kama mashine, magari na vifaa vingine.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Makampuni ya GSM, Benson Mahenya amesema wameamua kushirikiana na EFTA kutokana na kutambua umuhimu wa shughuli za uzalishaji wanazozifanya pamoja na wateja wao.
Mahenya amesema kupitia mkataba huo, mawakala na wadau wanaosambaza bidhaa zao ambao wanakosa mikopo kwa vigezo vya kawaida wataweza kupata mikopo ya magari kutoka EFTA kupitia dhamana yao.
“Naamini kwa kufanya hivi tutagusa maisha ya kila mtu na kuongeza thamani ya biashara wa wadau wetu na kuongeza msaada,”
Ameeleza kuwa kutokana na shughuli nyingi wanazofanya ikiwamo usalishaji wa vinywaji, pia wamejikita zaidi katika kuimarisha usafirishaji wa matunda kama malighafi ili kuondoa uharibifu.
“Sisi tumeona ni vyema tukaimarisha usafirishaji wa matunda kwa kwenda eneo la uzalishaji ili yasiharibike na kupotea pia kumpa thamani mkulima,” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo na Masoko wa EFTA Tanzania, Clerius Asiel amesema kwa zaidi ya miaka 20 wamekuwa nguzo muhimu kwa wafanyabiasha wadogo na kati nchini kwa kuwasidia kumiliki mashine na magari kwa mikopo nafuu bila dhamana.
Ameeleza kuwa mkataba huo na GSM umekuja baada ya kuwezesha upatikanaji wa magari zaidi ya 60 ya kusambaza bidhaa za kampuni hiyo.
” Hatua hii ni kielelezo cha maono yetu ya pamoja ya kukuza biashara endelevu, huku tukiwa na mchango wa moja kwa moja katika uundaji wa ajira na kuboresha kipato kwa wafanyabiashara wadogo.
” Kwa kuingia makubaliano haya GSM wanatupa nafasi ya kufanya biashara na wadau wao wote. Yaani leo hii kama ni mdau wa GSM ukihitaji kifaa chochote cha kusaidia katika biashara yako, taasisi ya EFTA itakupatia mkopo kuanzia wa mwaka mmoja hadi miaka mitatu,” amesema Asiel.
Amefafanua kuwa kwa mwaka jana pekee wameweza kutumia zaidi ya bilioni 48 kwa wakulima, wafanyabiashara na wajasiliamali.
Aidha ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 20 wamefanikiwa kuwakopesha wajasiliamali 100,000 ambapo kiasi cha fedha walichotumia kinafikia Sh. 250 bilioni.
ZINAZOFANANA
NIDA kusitisha namba ya utambulisho Mei Mosi
Dk. Mpango: Tuweke mikakati ya kukuza mapato ya ndani
Meridianbet yawakuna wapenzi wa Aviator PS5 yang’aa kwa mshindi wa juu