
PZG-PR imetunukiwa tuzo ya ‘Best PR Agency 2024’ nchini Tanzania katika Tuzo za Umahiri wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Mwaka 2024 zilizofanyika Jumamosi, 29 Machi 2025, ambazo zinazotolewa na ‘Public Relations Society of Tanzania’ (PRST). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
PZG-PR imepokea tuzo hii ya kitaasisi kwa mara ya kwanza ikiwa ni hatua muhimu ya mafanikio yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu ilipoanza kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu katika mawasiliano ya kimkakati ili kuleta matokeo chanya kupitia ubunifu kwenye sekta ya mawasiliano na uhusiano wa umma nchini Tanzania.
Ikiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Prudence Zoe Glorious, PZG-PR imejijengea sifa kupitia ubunifu na dhamira thabiti ya kutoa huduma katika sekta ya uhusiano wa umma. Katika kipindi chote, PZG-PR imejitanabaisha kama kinara katika kutoa huduma bora kwenye sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki.
Mpaka sasa, PZG-PR imeweza kutoa huduma kwa wateja mbalimbali ikiwemo:- UNICEF Tanzania, Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Shirika la Ndege la Jambojet, IYF & MasterCard Foundation, Aga Khan Foundation, Segal Family Foundation, Benki ya Stanbic Tanzania, Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, na AGRA.
“Tuzo hii ni inatukumbusha kuendeleza jitihada zitakazotufanya tukue zaidi, tujifunze zaidi, kuwa wabunifu zaidi ili kuwa bora zaidi, sio tu katika mikakati na ubunifu, bali pia kama kampuni inayokuza fikra na maarifa zaidi. Tunamshukuru Mungu, timu yetu ya wafanyakazi, washauri wetu wataalam, walezi wetu, watu wanaojitolea, wateja, pamoja na wale wote waliotuunga mkono katika mafanikio haya,” amesema Prudence Zoe Glorious.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, PZG-PR imeweza kutekeleza kampeni muhimu na matukio makubwa ya kihistoria kama vile uzinduzi wa hati fungani ya kwanza ya kijani (Tanga Water Green Bond) katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Uratibu na Usimamizi wa Wiki ya AZAKI 2024, pamoja na uzinduzi wa safari ya kwanza ya Jambojet kati ya Zanzibar na Mombasa.
ZINAZOFANANA
TRA yawashukuru Wahariri kwa kuhamasisha ulipaji kodi
TEF yawarejesha tena Balile, Machumu
STAMICO kuendeleza leseni za uchimbaji dhahabu Kigosi