April 5, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Puma Energy Tanzania yachangia mitungi ya gesi uzinduzi wa Mwenge Mkuranga

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega (wa pili kushoto) akipotea msaada wa mitungi ya gesi

PUMA Energy Tanzania imeshiriki katika shughuli za za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani, ambazo ziliongozwa na Waziri wizara ya Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Hadija Nasri Ali, na Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Ismail Ussi Ali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Kampuni iliwakilishwa na Meneja Mauzo Gesi Puma Energy, Erick Meena, ambaye alikabidhi mitungi ya PumaGas kwa Ulega kama ni sehemu ya jitihada za Puma Energy Tanzania kuunga juhudi za serikali katika kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa uhakika na gharama nafuu nchini kote.

Hivi karibuni kampuni ya Puma Energy Tanzania ilizundua upatikanaji wa huduma ya PumaGas jijini Dodoma na kuongeza wigo wake kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Ikiwa ni jitihada za uungaji mkono wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024 2034), uliozinduliwa Mei 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia jijini Paris ulioandaliwa na Shirika la Nishati Duniani (IEA).

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Hadija Nasri Ali, akizungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani

Sasa wateja wanaweza kununua mitungi ya gesi katika vituo vyote vya huduma za kujaza mafuta Dodoma, pamoja na mawakala wa uuzaji wa rejareja. Kampuni pia inatarajia kuzindua maduka mawili ya kisasa ya PumaGas ambayo yatatoa huduma za kisasa, yakiwa na huduma mbalimbali ikiwemo kujaza na kubadilisha mitungi ya gesi, kuhakikisha watu hawakwami katika shughuli zao za kila siku.

Kama hiyo haitoshi, kwa kuanza rasmi upatikanaji wa huduma hii mpya jijini Dodoma, wateja watapatiwa ofa mbalimbali pindi wanunuapo mitungi ya gesi ya ujazo tofauti kama vile 6kg, 15kg, na 38kg.

Kwa kuongezea, pia kampuni inategemea kuzindua huduma ya uuzaji wa uuzaji wa nishati kwa wingi au ujazo mkubwa kuanzia 200kg mpaka 20,000kg.

About The Author

error: Content is protected !!