April 3, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wizara ya Afya kuchunguza sakata la mama kubadilishiwa mtoto

Waziri wa Afya, Jenister Mhagama

 

WIZARA ya Afya kupitia kitengo cha mawasiliano serikalini imemsimamisha kazi muuguzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, aliyemhudumia Neema Kilugara aliyedai kubadilishiwa mtoto aliyejifungua hospitalini hapo. Anaripoti. Apaikunda Mosha. Arusha … (endelea).

Taarifa hiyo iliyotolewa leo tarehe 2 Aprili 2025, inaeleza kuwa mzazi huyo anatambulika kwa jina la Neema Kilugala alidai kuwa baada ya kujifungua alioneshwa mtoto wake na muuguzi  akiwa ni mzima.

Hata hivyo aligundua kuwa amebadilishiwa mtoto wake baada ya kuletewa mtoto akiwa amefungwa na vitenge ambavyo si vya kwake.

Kwa mujibu wa taarifa muuguzi wa hospitali hiyo alidai kuwa alichanganya vitenge na vya mtoto mwingine hivyo akaahidi kwenda kubadilisha pamoja na kuchukua hatua hiyo bado kulikuwa na hali ya sintofahamu.

Hivyo kufuatia hali hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha na Jeshi la Polisi imechukua hatua  ya  kuchukua sampuli za wazazi waliojifungua kipindi hicho pamoja na za watoto kwa ajili ya chunguzi wa vinasaba (DNA) katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa baada ya chunguzi kukamilika taarifa rasmi zitatolewa na hatua stahiki zitachukuliwa.

About The Author

error: Content is protected !!