April 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waumini wa Dini ya Kiislamu wapewa mwongozo

 

WAHUMINI wa Dini ya Kiislamu nchini wametakiwa kuhakikisha wanasimania misingi ya upendo,Amani na Ushirikiano sambamba na kusimamia amani ya nchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Katibu wa Sekretariet Baraza la Ulamaa Taifa, Sheik Swed Twaibu Swed, kwa niaba ya Muft Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuber wakati wa Ibada ya sherehe ya sikukuu ya Eid ul- Fitr iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Sheikh Swed kwa niaba ya Muft wa Tanzania amesema kuwa waumini wa dini hiyo wanatakiwa kutambua kuwa wanayo kazi kubwa ya kulinda amani ya nchi na kuliombea taifa ili kuendelee kuwepo kwa amani na utulivu.

Akizungumzia suala la uchaguzi amesema kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha anakuwa mlinzi na balozi mwema wa kuhubiri amani ya nchi hususani wakati uchaguzi.

“Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kuwachagua wabunge,madiwani na Rais kwa maana hiyo ni wajibu wa kila mtanzania kusimama imara kuhakikisha amani na utulivu vinatawala.

“Tusikubali kugawanyika kwa namna yoyote ile na badala yake tushikamane kwani Tanzania ni yetu na sisi ndio watanzania wenye jukumu la kuitunza Tanzania kwa ajili ya vizazi vijavyo,” ameeleza Sheik Swed.

Kwa kwa upande wake Sheikh Lali Abdul’Azizi, Imam Masjid Bilaly Area C Jijini Dodoma,amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kuitumia sikukuu hiyo kutafakari mambo Makuu ambayo Mungu amewatendea.

Pia amesema wasitumie sikukuu hiyo kufanya anasa au kutumia vyakula na vinywaji ambavyo Mungu ameviharamisha.

About The Author

error: Content is protected !!