April 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanawake wasiojistiri vyema ni wachafu

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaji Dk.Mustapha Shaban Rajabu

 

SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma Alhaji Dk.Mustapha Shaban Rajabu amewakemea baadhi ya wanawake ambao wanajipamba kinyume cha maagizo ya Mungu na kuvaa nguo za kuonesha maumbile yao na kusema kuwa kwa kujipamba huko ni sawa na uchafu au kujipaka matope. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ametoa kemeo hilo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya Eid al-Fitr iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma kwa kueleza kuwa kwa sasa wapo wanawake ambao wameacha maadili ya kimungu na kufanya mambo yao wenyewe hususani wakati wa kujipamba na kuvaa mavazi yasiyo na starah.

Amesema mwanamke ambaye anajibandika kope,nywwle bandia (mawigi)kujichubua kwa kujiongezea weupe,kuvaa nguo za aibu za kuonyesha maumbile ni sawa na kujipaka uchafu katika mwili na wawapo kwenye ibada hawawezi kupata thawabu.

“Katika dini ya Kiislamu sheria inaweka wazi kwa kumtaka mwanamke kuvaa nguo za kujistiri mwili wake na kwa sheria hiyo inasema mwanamke anapokuwa ajajistiri vyema ni sawa kama yupo uchi kwa maana sehemu ambayo haihesabiki kuwa uchi kwa mwanamke ni usoni na vijanja viwili vya mikono.

“Lakini iwapo ataacha kifua wazi,tumbo,kitovu au kuvaa nguo zinazoonesha maumbile yake huyo mtu ni sawa na aliye uchi kwa kuwa tayari sheria za Dini ya Kiislamu zinamkataza,” ameeleza Sheikh wa Mkoa wa Dodoma.

Amesema mwanamke anasitilika kwa kuvaa mavazi marefu na kuchora ina au piko na achorwe na mumeo na kuonwa na mumewe tu hayo maua.

Hata hivyo amesema sheria ya Dini ya kiislamu inawazuia wanaume kuvaa mavazi ya kubana na kuonesha maumbile,kusuka nywele,kuvaa nikuku au kuvaa milegezo au namna yoyote ya mavazi yampasayo mwanamke.

Amesema mwanaime wa aina hiyo ni machukizo mbele za Mungu na kwa kufanya hivyo Dini ya kiislamu inamuona kama mwanaume huyo ni filauni.

About The Author

error: Content is protected !!