
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuna haja ya kurekebisha Sera katika sheria za uagizaji wa magari ili kulinda viwanda vya utendenezaji magari nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).
Prof. Kitila ameyasema hayo wakati leo tarehe 27 Machi 2025, alipotembelea kiwanda cha kutengeneza magari nchini cha GF Vehicle Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Akiwa ameambatana na viongozi wa TCI, Waziri Mkumbo ametembelea kiwanda hicho na kujionea namna kinavyounganisha magari hayo kuanzia hatua ya mwazo hadi linakamilika na alifanikiwa kushuhudia uzinduzi wa gari ya 3400 ikiwa ni toka kuanzishwa kwa kiwanda hicho.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho , Ezra Mereng amewasilisha hoja ya maombi kwa serikali ya kubadilishwa kwa sera na sheria za uagizaji wa magari nchini ili kulinda viwanda vya ndani.
Amesema wao kama kampuni wanafanya upanuzi wa kuingia awamu ya 3 ambayo inategemewa kufanya uwekezaji wa mtaji wa zaidi ya sh 10 bilioni na hadi sasa imeajiri zaidi ya vijana 200 na katika awamu ya 3 wanatarajia kuajiri zaidi ya vijana 300 wa ajira ya moja kwa moja.
Katika awamu hii tunahitaji vitu vingi vipatikane nchini kama chuma na vifaa vingine kwa mfano, tumeshaanza kununua betri za magari kutoka katika kiwanda kimoja wapo nchini sasa bila kufanyika kwa mabadiliko ya sheria za kulinda viwanda vya ndani ni kazi bure.
“Kwa sasa kumekuwa na uagizaji holela wa magari na katika hili Tanzania tunakuwa walaji wa mwisho kwa kuwa magari mengi ni ya mtumba (used), pia kukiwa na sheria ya manunuzi na usimamizi kwa miradi mikubwa ya nchi basi lazima magari au vifaa vitakavyotumika vinunuliwe nchini hii itasaidia kuvilinda viwanda vyetu,” ameeleza Ezra.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yawafikia wanawake wajane Magomeni
Waziri Biteko ahimiza mabadiliko Jeshi la Magereza
Serikali: Faida itokanayo na uwekezaji ifikie zaidi ya asilimia 10