March 30, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tanesco yajivunia kudhibiti upotevu wa umeme

 

SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) limesema kuwa kati ya mafanikio makubwa ambayo shirika hilo linajivunia kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozo wa Rais Samia Hassan ni kudhibiti upotevu wa umeme kutoka asilimia 15.3 kwa mwaka 2021 hadi asilimia 14.54 kwa mwaka 2025. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …(endelea)

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo – Hanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Amesema kuwa Shirika hilo lilikuwa likikumbana na upotevu wa umeme kwa kiwango hicho lakini kutokana na juhudi za serikali iliyopo madarakani imefanikisha kupunguza upotevu wa umeme njiani.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa hatua ya kupunguza upotevu wa umeme inaongeza tija ya matumizi ya nishati hiyo kuwa ya uhakika na kurahisisha shughuli za watumiaji wa nishati hiyo muhimu.

Katika hatua nyingine muhimu amabayo shirika limejitapa nalo kuwa ni sehemu ya mafanikio ni pamoja na kuongezeka kwa vituo vya kupokea na kupozea umeme kutoka vituo 128 kwa mwaka 2021 hadi kufikia vituo 139 kwa mwaka 2025 sawa na ongezeko la vituo vya kupozea umeme 11.sawa na silimia 9.

Amesema kuwa hatua hiyo ni hatua kubwa ambayo inatoa urahisi wa kutoa umeme mkubwa sehemu moja na kuupeleka katika vituo vya kupozea umeme na kuwa tayari kwa mlaji au mtumiaji.

Mkurugenzi mtendaji mkuu huyo akiendelea kuelezea mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha miaka hiyo 4 amezitaja sababu za kukatika kwa umeme katika treni ya mwendakosi (SGR) kwa maelezo kuwa ni changamoto za ugeni wa kuwepo kwa usafiri huo nchini.

Hata hivyo ameaema kuwa ili kumaliza changamoto hiyo Shitika lipo mbioni kuanzisha Mkoa maalumu kwa ajili ya kushughulikia changamoto za umeme katika treni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Mpango wa Shirika ni SGR kuwa Mkoa ili kuweza kutatua changamoto na watakuwa na Meneja Uratibu ambaye atakuwa akishughukia mradi huo pekee ambaye atakuwa na timu maalumu.

Amesema uanzishwaji wa Mkoa maalumu wa SGR utakuwa na timu maalumu ambayo kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika muda wote.

Kuhusu kukatikatika kwa umeme nchini ,Mkurugenzi huyo Mtendaji amesema sababu kubwa ni kuzidiwa kwa gridi ya Taifa kutokana na ongezeko la watumiaji wa umeme huku akidai Shirika limejipanga kuhakikisha umeme unapatikana katika kila eneo nchini.

Amesema kwa kipindi cha mwaka 2021 wateja walikuwa milioni 3.1 na kufikia mwaka 2025 wateja ni milioni milioni 5.39 sawa na takribani ongezeko la wateja wapya milioni 2.2 ndani ya miaka 4 sasa.

About The Author

error: Content is protected !!