March 30, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mwenezi Bawacha ashambuliwa mlinzi, Polisi wafunguka

 

MWENEZI wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Taifa Sigrada Mligo ameripotiwa kujeruhiwa na mlinzi wa kikao cha ndani kilichokuwa kikiongozwa na viongozi wa CHADEMA Taifa wakiongozwa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche kilichokuwa kikifanyika mjini Njombe March 25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Njombe … (endelea)

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema,

Shambulio la kudhuru mwili alilolipata Katibu Mwenezi wa Bawacha Taifa ambaye amefahamika kwa jina la Sigrada Mligo 34, mkazi wa Mji mwema mkoa wa Njombe.

Mnamo tarehe 25.03.2025 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilikuwa na kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Taifa wakiongozwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche.

Amesema katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo lililokuwa linamuhusu Katibu Mwenezi wa Bawacha Taifa, Sigrada Mligo juu ya kufanya mikutano bila kufuata utaratibu wa chama hicho.

Banga amesema Katika hoja hiyo, kuliibuka taharuki na sintofahamu na baadae alielekezwa kutolewa nje. ya kikao ili kupunguza munkali aliyokuwa nayo.

Aidha amesema baada ya kuwa hali imetulia yalitoka maelekezo ndani ya kwamba aweze kurejea na kikao hicho kiweze kumalizika lakini chakushangaza mmoja wa walinzi wa chama hicho cha CHADEMA aliyefahamika kwa jina Noel Olevale aliweza kumshambulia Sigrada Mligo na kuweza kuanguka chini wakati wa tukio hilo kulikuwa na askari pembeni ambao walichukua hatua ya kutaka kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo aliponyoka na kukimbia.

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe lilifanya jitihada za kumpatia huduma ya kwanza ikiwemo kumpatia PF3 na kufungua kesi na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Kibena mkoani Njombe akiwa anaendelea kupatiwa matibabu na jitihada za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.

Hata hivyo Banga amesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani halitosita kuchukua hatua kwa mtu yoyote atakayebainika.

Vilevile amesema hali ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Njombe ni shwari mikutano ya Chadema inaendelea kufanyika na hakuna uvunjifu wa amani.

About The Author

error: Content is protected !!