
KAMPUNI ya GF Trucks kupitia kampuni ya GF Automobile imeingia makubaliano na Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NaCoNGO ), yakilenga kunufaisha pande zote mbili katika nyanja mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks, Mujtaba Karmali amesema wao kama wauzaji wa magari na mitambo wameoana kuna haja ya kuingia makubaliano hayo ya kimkakati ambapo pia watatoa elimu, kuwajengea uwezo na uelewa katika maeneo tofauti.
Aidha Karmali amesema tayari wao wameanza mpango wa kutoa mafunzo kazi kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali mfano, VETA na DIT ili kuwajengea uwezo wa kuweza kufanya kazi na kupata uzoefu kazini.
“Makubaliano haya yatarahisisha kuwafikia makundi ya vijana nchi nzima na kuungana na serikali katika mpango wa kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri kwa kupita katika vyuo mbalimbali,” ameeleza Karmali.
Nae Mwenyekiti wa NaCoNGO, Jasper Makala ameishukuru kampuni ya GF Trucks kwa kuonyesha njia kwa makampuni ya Kitanzania kuchangia maendeleo ya jamii kupitia mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.
Amesisitiza kuwa ushirikiano na makampuni binafsi ya ndani ya nchi ni mbinu mojawapo ya kupunguza utegemezi toka nje ya nchi kuelekea katika uendelevu wa mashirika.
ZINAZOFANANA
Waziri Biteko ahimiza mabadiliko Jeshi la Magereza
Serikali: Faida itokanayo na uwekezaji ifikie zaidi ya asilimia 10
Shirika la Posta limezalisha hasara ya 23.63 bilioni kwa mwaka – CAG Kichere